[caption id="attachment_26185" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usajili wa na Utoaji wa Namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi TIN lililofanyika katika eneo la Chanika, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam leo.[/caption]
Na: Mwandishi Wetu - MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa inatarajia kusajili walipakodi wapya takribani 1000,000 ambao kwa pamoja wanakadiriwa kuwa wataongeza mapato ya tokanayo na kodi kwa kiwango cha Sh. Bilioni 1.5 kwa mwaka.
Akizungumza wakati wa zoezi la usajili wa wafanyabiashara wadogo zoezi lilionza leo katika Eneo la Chanika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wadogo ni endelevu.
[caption id="attachment_26186" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usajili wa na Utoaji wa Namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) lililofanyika katika eneo la Chanika, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam leo.[/caption]" Zoezi hili la usajili wa walipa kodi ni endelevu, lengo letu kama Mamlaka ya Kodi Tanzania ni kuhakikisha tunawasogezea huduma wateja wetu lakini pia tunatimiza wajibu wetu wa kukusanya kodi." Alisema Mwandumbya.
Aidha Mwandumbya alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ili waweze kusajiliwa kama walipa kodi na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN).
Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara.
[caption id="attachment_26188" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wakazi wa Chanika katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam wakipata maelekezo kutoka kwa Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa zoezi la Kusajili na Kutoa Namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) zoezi lilioanza leo.[/caption] [caption id="attachment_26189" align="aligncenter" width="750"] Mfanyakazi wa TRA Bi. Regina Urio akichukua taarifa za mmoja wa wakazi wa Chanika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam aliyefika katika kituo cha kusajilia walipa kodi wapya zoezi lililoanza leo jijini Dar es Salaam.[/caption]Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo Richard Kayombo amewataka wananchi wanaoishi Chanika na maeneo jirani ikiwemo Mvuti kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha na kusema kuwa zoezi hilo katika Kituo hicho litadumu kwa muda wa siku tano hivyo ni vyema wakatumia fursa hiyo kupata huduma hiyo inayotolewa bure.
"Usajili wa walipa kodi katika eneo hili la Chanika utadumu kwa siku tano, baada ya hapo tutahamia maeneo ya Tababata Segerea na Kisukuru, na kisha zoezi litaendelea Manispaa ya Temeke na baadaye Kinondoni huku tukifungua vituo katika maeneo mbalimbali," alisema Kayombo.
[caption id="attachment_26190" align="aligncenter" width="750"] Mfanyakazi wa TRA Bi. Gloria Magunguli akifanya uhakiki wa taarifa za mmoja wa wakazi wa Chanika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam aliyefika katika kituo cha TRA Kilichowekwa katika eneo la Kituo Kipya cha Polisi Chanika kwa ajili ya kusajilia walipa kodi wapya zoezi lililoanza leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Shija - MAELEZO)[/caption]Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni hii baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa wafanyabiashara kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi Vingunguti.
Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na matapeli kwani kazi hiyo inafanya na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa kazi hiyo.