Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TOSCI Yatoa Mafunzo kwa Wafanyabiashara ya mbegu 1,832
Aug 15, 2023
TOSCI Yatoa Mafunzo kwa Wafanyabiashara ya mbegu 1,832
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI), Patrick Ngwediagi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi anayoisimamia na mwelekeo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 15, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeweza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa mbegu 1,832 na kusajili wafanyabiashara 1,031 ikiwa na lengo la kuhakikisha wakulima na wadau wengine wa mbegu wanazouza kwa wananchi ni sahihi kwa matumizi.

Hayo yameelezwa leo Agosti 15, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. Patrick Ngwediagi katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma alipokuwa akieleza utekelezaji wa bajeti ya taasisi hiyo katika mwaka huu wa fedha 2023/24.

“Jukumu kubwa na TOSCI ni kusimamia shughuli za uzalishaji wa mbegu na biashara ya mbegu ili kuwahakikishia wakulima na wadau wengine kuwa mbegu wanazouziwa ni sahihi kwa matumizi hivyo TOSCI imepewa majukumu mbalimbali ikiwemo kusajili wafanyabiashara au wazalishaji wa mbegu ” amebainisha Bw. Ngwediagi.

Aidha amesema kuwa TOSCI imeimarisha na kuanzisha ofisi za kanda ili kutoa huduma zake kwa wadau kwa karibu zaidi, Ofisi za Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kusini zimefunguliwa wakati Ofisi za Kanda ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini zimeboreshwa na kupatiwa watumishi zaidi.

Akizungumza kuhusu usajili na ukaguzi wa mashamba ya mbegu, Bw. Ngwediagi amesema kuwa idadi ya mashamba ya mbegu 1,554  yamesajiliwa na kukaguliwa kwa mwaka 2022/2023.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi