Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Toka Tupate Uhuru, Hatujawahi Kuuza Kahawa Tani 82,000 Nje ya Nchi - Mhe. Bashe
Aug 08, 2023
Toka Tupate Uhuru, Hatujawahi Kuuza Kahawa Tani 82,000 Nje ya Nchi - Mhe. Bashe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera wakati akiangalia video fupi ya masuala ya Kilimo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Na Jonas Kamaleki - Mbeya

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussen Bashe amesema kuwa tangu Tanganyika ipate uhuru haijawahi kutokea kuuza kahawa tani 82,000 nje ya nchi lakini mwaka huu imeuza kahawa tani 82,000, nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Waziri Bashe haya ni mapinduzi Makubwa katika Kilimo.

"Sekta ya kilimo inajengwa na sekta ya umma, Binafsi na Taasisi za maendeleo za kimataifa, nashukuru USAID kwa kurudisha mradi wa "Feed the Future"  na sasa tutaanza utekelezaji kwa mradi wa dola milioni 24 katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. 
Nawashukuru pia Benki ya Maendeleo ya Afrika ( AfDB) ambao tunatengeneza nao mpango wa utekelezaji wa mradi wa BBT wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 151," alishukuru Waziri Bashe.

Miongoni wa wanufaika wa mradi huo wa BBT ni Mkoa wa Njombe ambako kutajengwa mradi wa umwagiliaji ( block Farm) ekari 87,000 na Mkoa wa Mbeya Wilayani Chunya ambako nako kutajengwa Block Farm yenye ekari 57,000.

Alifafanua kuwa mpaka sasa wakulima wameuza mazao zaidi ya dola milioni 240 na asilimia 80 wamashalipwa hela zao na tarehe 15 mwezi huu waliobaki watamaliziwa hela zao.

"Mhe. Rais, mwaka mmoja uliopita ulihamasisha uwekezaji katika sekta ya tumbaku na mwaka huu uzalishaji umepanda kutoka tani 65,000 hadi tani 120,000," alisema Mhe. Bashe.

Uzalisha wa chakula kabla ya mbolea ya ruzuku msimu wa 2021/ 2022 ulikuwa tani milioni 17 lakini baada ya mbolea ya ruzuku kuja wakulima wamezalisha tani milioni 2, 042, 114.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi