Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TFDA Yafungia Machinjio 26 Dar
May 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Frank Mvungi Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefunga jumla ya machinjio 26 kati ya 55 yaliyokaguliwa katika Mkoa wa Dar es Saalam kufuatia ukaguzi uliofanywa kati ya mei 2 hadi 12,2017 katika Manispaa za Kinondoni,Ilala,Ubungo na Temeke. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mkuu wa TFDA bw. Hiiti Sillo amesema machinjio zilizokaguliwa ni za ngombe,kuku na nguruwe lengo likiwa ni kuangalia utekelezaji wa sheria ya Chakula,Dawa na Vipodozi Sura 209 hususan kukagua majengo,miundo mbinu,mfumo wa uchinjaji,uendeshaji wa machinjio kama unazingatia kanuni za usafi na mazingira. Akifafanua Sillo amesema kuwa machinjio mbili za ngombe ambazo ni Vingungiti na Mazizini za Manispaa ya Ilala zimepewa muda wa siku saba kurekebisha mapungufu yaliyobainika hususan uuzwaji wa nyama ndani ya machinjio,uchinjaji usiozingatia uwezo wa machinjio na udhibiti wa watu wasiohusika kuingia ndani ya machinjio. “Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) itaendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda Afya ya Jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya Chakula,Dawa,Vipodozi, na Vitendanishi” Alisisitiza Sillo Akizungumzia ufungaji wa machinjio hizo Sillo amesema kuwa Kati ya Machinjio zilizofungwa 1 ni ya ngombe,14 za nguruwe ,11 za kuku kutokana na kukiuka sheria ya chakula Dawa na Vipodozi sura ya 219 na pia kanuni za usafi. Pia Sillo alishukuru Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,Bodi ya Nyama,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Salaam, na Ofisi za Afya na Mifugo za Manisapaa za Ilala,Temeke,Ubungo na Kinondoni kwa Kushiriki kikamilifu katika ukaguzi huo. Aliongeza kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na vyombo vingine vilivyoshiriki katika Ukaguzi huo inawaelekeza wamiliki wa machinjio zilizofungwa kufanya marekebisho ya mapungufu yaliyobainika ikiwa ni pamoja na kuchukua ramani zilizotolewa na Bodi ya Nyama katika ujenzi wa machinjio yao ili kuendana na matakwa ya sheria za nchi. Aidha TFDA kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya nyama inaendelea kuchukua hatua mbalimnbali katika kuandaa mpango mkakati wa kuimarisha machinjio nchini ili zote ziwe na viwango vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa mujibu wa sheria ya chakula,Dawa na Vipodozi,sura 219 ina jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa Chakula,dawa,Vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya za wananchi.  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi