[caption id="attachment_29081" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelis Mafumiko akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Bahi Mkoani Dodoma Bw. Emmanuel Dickson wakati wa ziara yake yakukagua mradi wa kuwajengea uwezo wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi unaotekelezwa katika Wilaya hiyo mapema wiki hii.
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unawajengea wasichana na wanawake walioolewa katika umri mdogo kuwa na uelewa, ujuzi na stadi za maisha katika elimu, ufundi na ujasiriamali utakaowawezesha kushirki katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa wa Taifa umeanza kuonesha mafanikio katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuona utekelezaji wa mradi huo katika wilaya hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa ameridhirishwa na maendeleo ya mradi huo ambao lengo lake ni kuwajengea uwezo wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba na ndoa za utotoni.
[caption id="attachment_29083" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelis Mafumiko akisisitiza jambo wakati akikagua miundo mbinu inayotumika kuwajengea uwezo wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi Wilayani Bahi.Kushoto ni Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bahi Bw. Aniseti Gervas.[/caption]“ Nimefurashishwa na mwitikio wa wasichana katika Wilaya hii ikiwa ni dalili njema kuwa matokeo ya mradi yameanza kuonekana kwa kuwa wasichana hawa watakuwa na uwezo wa kujitambua na kujiajiri baada ya mafunzo haya yatakayowajengea uelewa,ujuzi na stadi za maisha ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ” Alisisitiza Dkt. Mafumiko.
Naye Mkufunzi Mkazi wa Taasisi hiyo mkoa wa Dodoma Bw. Habibu Muyula amesema kuwa wasichana hao wanafundishwa masomo ya nadharia na vitendo ili kuwapa uwezo wa kujitegemea na kuendesha maisha yao hivyo kutokuwa tegemezi.
“Baada ya muda si mrefu mtaanza kujifunza namna ya kutengeneza batiki, sabuni na bidhaa nyingine, na hivyo kuweza kuunda vikundi vya uzalishaji vitakavyowasaida kupata mitaji ya kuboresha maisha yenu” Alisisitiza Bw. Muyula.
[caption id="attachment_29084" align="aligncenter" width="800"] Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu (TEWW) Dodoma Bw. Habibu Muyula Akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo Wilayani Bahi wakati wa Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelis Mafumiko kukagua maendeleo ya mradi huo.Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bahi, Augustino Ndonu amesema kuwa mradi huo ni ukombozi kwa mtoto wa kike katika wilaya hiyo na kuipongeza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kutoa fursa kwa wilaya ya Bahi.
Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unatekelezwa wilaya za Bahi Kongwa, Nkasi na Kalambo katika mikoa ya Dodoma na Rukwa kwa ushirikiano wa Shirika la Elimu la Jumuiya ya Madola na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.