Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS Yatoa Elimu kwa Wanafunzi 10, 757 Dar, Pwani na Morogoro
Nov 05, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu

 WANAFUNZI 10,757 wa shule tisa zasekondari na msingi katika mikoa yaDar es Salaam, Morogoro na Pwaniwamepatiwa elimu ya viwangoiliyotolewa na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) itakayowasaidiakuwa mabalozi wa viwango ndani yajamii.

Maofisa hao walitoa elimu hiyo wiki iliyopita kwenye mikoa ya Dar esSalaam, Pwani na Morogoro ikiwa nisehemu ya Maadhimisho ya Siku yaViwango yaliyoadhimishwa na shirikahilo kuanzia Oktoba 21 hadi 31, mwakahuu.

Maadhimisho hayo huadhimishwa naShirika la Viwango la Kimataifa (ISO) ambalo TBS ni mwanachama kila mwakaifikapo Oktoba 14, lakini kwa Tanzania kutokana na siku hiyo kuangukia tareheya kumbukizi ya kifo cha Baba wa TaifaMwalimu Julius Nyerere, TBS ilisogezambele maadhimisho hayo hadi kuanziaOktoba 21 na Oktoba 31, mwaka huu.

Shule ambazo wanafunzi wake walipatiwaelimu hiyo kwa mkoa wa Morogoro niKayenzi, Kilakala, Kihonda, Chief Albert, Mwere A, Bungo, huku katikamkoa Pwani elimu hiyo ikiwa imetolewakwa shule za Bundikani na Maendeleo.

Kwa Dar es Salaam elimu hiyo ilitolewakatika shule ya Kibasila. Akizungumzana waandishi wa habari kuhusiana naelimu hiyo, Ofisa Uhusiano wa shirikahilo, Neema Mtemvu, alisema walitumiamaadhimisho hiyo kutoa elimu kwawanafunzi hao kuhusiana na majukumu yashirika, umuhimu wa viwango, madharaya kutumia bidhaa zisizokidhi viwangona sababu za maadhimisho ya siku yaviwango duniani.

Mtemvu, aliwataka wanafunzi haokuhakikisha wanakuwa mabalozi wazurindani ya jamii kwa kuhakikishawanatumia bidhaa zenye alama ya ubora, kwani bidhaa zisizo na viwango zinamadhara makubwa kiafya.

Mtemvu aliwataka wanafunzi hao kuwamakini na kuhakikisha wanachunguzabidhaa kabla hawajainunua ilikujiridhisha kama zinakidhi viwango, kwani kufanya hivyo kutawasaidiakujiepusha na madhara yatokanayo nabidhaa zisizokuwa na viwango.

Alisema kuna madhara mengi yatokanayona bidhaa zisizokuwa na viwango, zikiwemo za kiafya.

Kwa mujibu wa Mtemvu wanafunziwaliopata elimu hiyo waliahidi kuwamabalozi kwa kuhakikisha bidhaazinazonunuliwa na wazazi na watuwengine ni zile zenye alama ya ubora.

Wakati wa mafunzo hayo wanafunzi haowalikuwa wakiulizwa maswali mbalimbalikuhusiana na viwango na waliofanywavizuri walipewa zawadi za ainambalimbali za vifaa vya shule ikiwemodaftari na mabegi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi