[caption id="attachment_27030" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.[/caption]
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.
Agizo hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo hayo ili kuvutia wapangaji wao.
"Wasimamizi wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa zimetelekezwa muda mrefu", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
[caption id="attachment_27031" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya nyumba 76 mkoani humo.[/caption]Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara, kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali. Amekemea tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TBA mkoani hapo, Edward Mwangasa, amekiri kutokuwa na hati kwa baadhi ya nyumba na viwanja wanavyovimiliki na hivyo amemuahidi Naibu Waziri huyo kuhakikisha anasimamia suala la utafutaji wa hati kwa nyumba hizo na viwanja vyote 128 walivyonavyo sasa. "Mheshimiwa Naibu Waziri nakuhakikishia kulifanyia kazi suala la ufuatiliaji wa hati za nyumba na viwanja ili kuweza kuepuka migogoro na wananchi wanaovamia viwanja vyetu", amesitiza Kaimu Meneja.
[caption id="attachment_27032" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.[/caption]Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amewataka wananchi kufuata sheria na kwamba hairuhusiwi kuvamia maeneo ya Serikali kwani maeneo hayo huwa yanatengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali.
Wakala wa Majengo Mkoani Mtwara una jumla ya nyumba 76 ambapo Manispaa ya mji wa Mtwara ina nyumba 64, Masasi 4, Nanyumbu 5 na Tandahimba 3 ambapo baadhi ya nyumba hizo zina hati na nyingine hazina.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano