[caption id="attachment_27674" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo , Mhe. Emmanuel Papian akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika miradi inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando.Mifugo na Kilimo, wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika miradi hiyo itakayowanufaisha wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji na Usambazaji maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani umefikia asilimia 72.2 ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Februari mwaka huu.
Hayo yamebainika hivi karibuni wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji, Mifugo, na Kilimo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Emmanuel Papian ambapo ziara hiyo ililenga kukagua miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na DAWASCO.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Papian alibainisha kuwa Kamati yake imeridhishwa na Kazi zinazotekelezwa na DAWASA katika mradi huo ambao utawanufaisha wananchi kwa kiwango kikubwa na kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji, baadhi ya maeneo hayo ni Salasala, Bunju,Wazo, Makongo, Mpiji, Zinga, Ukuni, Buma, Mataya, Mbezi Luis, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na maeneo yote yanayopata maji kupitia mtambo wa Ruvu juu.
[caption id="attachment_27675" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo,(kulia) akitoa taarifa ya utendaji kazi na utekelezaji wa miradi inayotekelzwa na DAWASA kwa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika miradi hiyo itakayowanufaisha wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Maeneo yaliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na eneo la ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhi maji la Changanyikeni, Salasala, Vituo vya kusukuma maji Makongo na Salasala.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA Bw. Laston Msongole amesema kuwa dhamira ya DAWASA ni kuhakikisha kuwa maeneo yote ambayo hayana huduma ya maji yanafikiwa yakiwemo yale ya Wilaya mpya ya Kigamboni.
"Tayari tumechimba visima virefu venye uwezo wa kuzalisha maji mengi katika eneo hilo hali itakayosaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji Kigamboni na kilichobaki ni kupata fedha za kujenga mfumo wa kusambaza maji hayo kwa wananchi" alisema Msongole.
[caption id="attachment_27677" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo wakipata maelezo Kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu wakati walipotembelea mtambo huo, Ruvu Mkoani Pwani.[/caption] [caption id="attachment_27678" align="aligncenter" width="750"] Mafundi wakiendelea na kazi ya kuchimba mtaro yatakapolazwa mabomba yatakayotumika kusambaza maji kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya mradi wa Uboreshaji na Usambazaji maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 72.2 na unatarajiwa kukamilika Februari mwaka huu.( Picha zote na DAWASA)[/caption]Katika kufanikisha mradi huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Romanus Mwangingo amebainisha kuwa kazi zinazotekelezwa kwa katika mradi huo wa Uboreshaji na Usambazaji huduma za maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa(9) ya kuhifadhia na kusambaza maji yenye ukubwa wa lita za ujazo milioni 3.0 hadi 6.0.
Kazi nyingine ni ununuzi na ufungaji wa pampu 16 kubwa za kusukuma maji, ununuzi wa Transfoma, ufungaji wa umeme wa msongo mkubwa, Aidha kazi hizo zitakwenda sambamba na ununuzi na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa jumla ya kilomita 477.
Mradi huu unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia DAWASA ulianza machi 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi februari mwaka huu na kunufaisha wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.