Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tasnia ya Sanaa Kuimarishwa ili Kuwanufaisha Wasanii
Aug 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46342" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini, mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Dianarose Shirima-MAELEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amekutana na wadau wa Sanaa mbalimbali nchini  katika kujadili maendeleo ya tasnia hiyo, zikiwepo  haki za wasanii na jinsi ya kuboresha tasnia ya Sanaa na muziki ili wasanii waweze kufaidika kwa kile wanachokifanya

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri Mwakyembe amesema kuwa Serikali ipo tayari kupokea mapendekezo ya wasanii kuhusu kuunganisha nguvu katika vyombo vya wasanii ambavyo ni COSOTA, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) NA Bodi ya Filamu Tanzania ili waweze kuhudumia wasanii kwa maendeleo ya kazi zao.

  [caption id="attachment_46344" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wanachama wa Chama wa Washereheshaji (SAA) wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam[/caption]

“Sisi tunawaletea mawazo tu, si Sheria, si Mswada ni mawazo ambayo yatamilikiwa na ninyi baada ya kuyapitisha”, na ninyi kama  wadau wa Sanaa na muziki waliohudhuria kwenye mkutano huu mntakia kutoa mawazo yenu  ili Tasnia hii iweze kufikia katika muafaka mzuri ambao utaboresha kazi za wasanii na kutetea maslahi ya kazi zao, Alisema Dkt.Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya Sanaa na Mziki imekuwepo muda mrefu na imekuwa kimbilio kwa vijana wengi, lakini imekuwa ikitajirisha baadhi ya watu na wengine kuachwa nyuma kimaendeleo, kwa hiyo mabadiliko katika Tasnia hiyo hayana budi kutokea ili kuleta ufanisi zaidi

Aliongeza kuwa mabadiliko hayo hayalengi kuvunja au kuingilia Mamlaka ya vyombo hivyo, bali lengo lake ni kusogeza huduma karibu kwa ajili ya kurahisisha kazi kwa wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini.

[caption id="attachment_46345" align="aligncenter" width="750"] Msanii wa Bongo Movie Nchini, Muhogo Mchungu akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46346" align="aligncenter" width="750"] Msanii wa Bongo Movie Nchini, Simoni Mwapagata akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46347" align="aligncenter" width="750"] Wasanii wa Bongo Movie, Shemsa Ford (kulia) na Jackline Wolper (kushoto) wakiteta jambo kabla ya Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, na Wasanii wa Sanaa zote nchini kuanza katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46348" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, akiandika mapendekezo anayoyasikia kuhusu mabadiliko ya Taasisi za Sanaa nchini katika Mkutano wake na Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini, mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)[/caption]  

Aidha Dkt.Mwakyembe alisema kuwa mabadiliko hayo yatafanya vyombo hivyo kuwa na lugha moja ili kuepuka wasanii kukamatwa au kufungiwa pale wanapokuwa wanafanya kazi zao kutokana na utofauti wa kanuni na Sheria zilizopo.

“Kipindi cha mabadiliko kimefika, watanzania tusiogope kufikiri katika tasnia hii, kwa muda mrefu imekuwa ikisaidia sana lakini haiwezi kuwafaidisha wachache na wengine wabaki masikini, haiwezekani ni lazima tufikirie njia itakayo tusaidia wote”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania, William Frank Chitanda, alisema kuwa Mabadiliko ya kuiunganisha Basata na Bodi ya Filamu ziungane na COSOTA ihamishiwe Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi