Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TANZIA: JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU TANZANIA MHE. UPENDO MSUYA AFARIKI DUNIA
Jul 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Upendo Msuya.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Upendo H. Msuya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 19/7/2017 katika hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa kuanzia Jana tarehe 18/7/2017.

Taarifa iliyotolewa na Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe, Ferdinand Wambali inasema Mahakama imepokea taarifa hizo za kusikitisha kutoka kwa familia ya Marehemu.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es salaam. Aidha, taratibu za mazishi zinafanywa na taarifa itatolewa hapo baadaye.

Marehemu Jaji Mstaafu Msuya alizaliwa tarehe 9 Desemba, 1957 katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania kama Hakimu tarehe 1 Januari, 1983.

Aidha, mwezi Oktoba mwaka 2007, Marehemu Msuya aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu.

Aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 24 Mei, 2008.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, Marehemu aliomba kustaafu kazi ambapo Mhe. Rais aliridhia uamuzi huo Mei 15, 2017.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi