Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the IMF– for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada (kulia), akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ambapo amesema kuwa uchumi wa Tanzania, katika kipindi cha Nusu ya Kwanza cha Mwaka (Januari hadi Juni, 2023), uchumi umekua kwa asilimia 5.3, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the IMF– for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Adriano Ubisse.
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa