Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yang’ara Suala la Amani Duniani
Mar 31, 2019
Na Msemaji Mkuu

Yaongoza Afrika Mashariki, Yawa 10 Bora Barani Afrika

Na Mwandishi Wetu

Taswira ya Tanzania kimataifa imeendelea kupaa baada ya Taasisi ya Global Peace Index (GPI) kuitangaza Tanzania kushika nafasi ya 51 miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2018.

Tanzania imeshika nafasi hiyo ikiwa ni ya juu zaidikufikiwa tangu mwaka 2010 na kuzishinda nchi kubwa duniani kama Marekani, China, Uingereza na Ajentina ambapo kwa Afrika ipo katika nafasi 10 bora na kuwa kinara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli iingine madarakani, Tanzania imekuwa ikipanda nafasi kila mwaka ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya 54, mwaka 2016 nafasi ya 58 na mwaka 2015 nafasi ya 64.

Kwa miujibu wa GPI, sababu zilizoipaisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa, mgawanyo sahihi wa rasilimali, upatikanaji huru wa taarifa, mazingira wezeshi ya biashara, uhusiano mzuri na nchi za jirani, kiwango cha rasilimali watu,  kuheshimu haki za watu wengine na ufanyaji kazi mzuri wa Serikali.

Nchi 71 zilikuwa na amani zaidi mwaka 2018 kuliko mwaka 2017”, inaeleza sehemu ya taarifa ya Global Peace Index na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi hizo 71 baada ya kushika nafasi ya 51 kulinganisha na nafasi ya 54 iliyoshika mwaka 2017.

Akitoa maoni yake juu ya kupaa kimataifa katika suala la amani, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbasi, kupitia akaunti yake yaTweeter, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuienzi amani ya Tanzania.

Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali amewapongeza wananchi na wadau wote waliotimiza wajibu wao katika kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani duniani.

Taarifa hii ya 12 kutolewa na Global Peace Index ambayo huzipima nchi 163 kulingana na hali ya amani katika nchi hizo. Taasisi hii inaongoza na kuheshimika katika masuala ya kwa kupima hali ya amani katika nchi mbalimbali duniani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi