Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kukutana na mgeni wake, Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantino ambaye alimtembelea ofisini kwake jana Februari 22, 2018 (Picha na Anitha Jonas-WHUSM).
Na Mwandishi Wetu.
Katika juhudi za kuhakikisha kuwa mchezo wa soka unaendelea na kuheshimika duniani, Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuliunga mkono Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ubadhirifu katika sekta ya michezo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameeleza hay oleo Februari 22, 2017 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa FIFA, Gianni Infantino ambaye alimtembelea Waziri Mkuu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantino akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Februari 22, 2018. (Picha na Anitha Jonas-WHUSM)
“Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli inaungamkono juhudi za FIFA za kupambana na rushwa na ubadhirifu michezoni”, alieleza Waziri Mkuu ambaye alimpokea Rais wa FIFA kwa niaba ya Rais.
Mheshimiwa Majaliwa alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua pia juhudi za Shirikisho hilo katika kuendeleza soka la vijana, wanawake na ubreshaji wa miundombinu ya mpira wa miguu.
Alilisisitizia Shirikisho hilo kuendelea kusimamia vema mchezo wa soka duniani na kutoa fursa zaidi kwa vijana katika ngazi mbalimbali ikiwemo shule za msingi, sekondari na hata vyuoni ikiwa ni sehemu ya mipango ya FIFA kuendeleza mchezo wa soka.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infoantino, kinyago aina ya Umoja kuashiria umoja kati ya Tanzania na Shirikisho hili. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Februari 22, 2018 ofisini kwa Waziri Mkuu (Picha na Anitha Jonas-WHUSM)
Waziri Mkuu pia alimshukuru Rais wa Shirikishola Soka Barani Afrika, Ahmed Ahmed kwa kazi nzuri ya kuendeleza soka barani Afrika na kumueleza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
“Tunakushukuru kwa kuleta fainali za mpira wa miguu kwa vijana barani Afrika kufanyika hapa Tanzania, Serikali imepokea kwa mikono miwili na imejiandaa kushiriki kikamilifu ikiwemo kushinda” alieleza Mheshimiwa Majaliwa.
Kwa uoande wake, Rais wa FIFA alimshukuru Waziri Mkuu na Watanzania kwa ujumla kwa namna ambavyo wamepata mapokezi mazuri na kumuomba Waziri Mkuu amfikishie salamu zake kwa Rais wa Jamhuriya Muunganowa Tanzania, Mheshimia John Pombe Magufuli.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa jezi ya FIFA ikiwa niishara ya kumkaribisha Waziri Mkuu katika Timu ya FIFA (Picha na Anitha Jonas-WHUSM)
Infantino ameeleza kuwa FIFA kushirikiana na Tanzaniakatika masuala ya michezo na Shirikisho hilo linaangalia namna ya kuisaidia Tanzania katika kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya soka katika mikoa tisa nchini kwa lengo la kusaidia kukuza mchezo wa mpira wa miguu nchini.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu wa Tanzania aliwakabidhi Rais wa FIFA na Rais wa CAF Kinyago cha Umoja kila mmoja ikiwa ni ishara ya umoja katika ya mashirikisho hayo mawili na Tanzania ambapo kwa upande wake, Rais wa FIFA alimkabidhi Mhesimiwa Majaliwa beji na jezi ya timu ya FIFA ili kumfanya kuwa sehemu ya timu hiyo.
Rais huyo wa FIFA aliwasili nchini jana alfajiri kwa ajili ya mkutano wa siku moja wa FIFA na anatarajiwa kuondoka
leo nchini kwa ndege binafsi.