[caption id="attachment_5506" align="aligncenter" width="736"] Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akitia saini kitabu cha wageni katika moja ya mabanda aliyotembelea katika maonesho ya sabasaba Katika Viwanja JK Nyerere,barabaraya kilwa Jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na: Frank Mvungi
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj. Ali Hassan Mwinyi amepongeza hatua iliyofikiwa katika kujenga Tanzania ya Viwanda itakayosaidia kukuza uchumi kwa kuzalisha ajira na kuongeza pato la Taifa.
Pongezi hizo zamaezitoa leo jijini Dar es Salaam alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonesho 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) -Sabasaba ili kujionea bidhaa na huduma zinazotolewa na washiriki wa maonesho hayo.
“Baada ya Kutembelea maonesho haya ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam nimeamini sasa kuwa Tanzania ya Viwanda inawezekana na tumeanza kuona utekelezaji kupitia maonesho haya ambayo ni mazuri na kila mwaka naona yanazidi kuboreshwa” alisisitiza Mzee Mwinyi
Akifafanua amesema kuwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwa sasa zina ubora unaodhihirisha kuwa nchi imeamua kujenga uwezo wake na kujitegemea katika kujenga uchumi wake na ustawi wa watu wake hali inayoonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa ya kiuchumi hapa nchini yanayolenga kuwainua watanzania wote hasa wa kipato cha chini.
[caption id="attachment_5509" align="aligncenter" width="750"] Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kutembelea maonesho ya sabasaba Katika Viwanja JK Nyerere, barabara ya kilwa Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE Edwin Rutagaruka[/caption]Naye Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akizungumza katika maonesho hayo amesema kuwa Mahakamama imejipanga vizuri katika kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa kuhakikisha kuwa haki inatolewa kwa wakati ikiwa ni sehemu ya maboresho ili kuongeza tija.
“Tumeamua kushughulikia kesi zote kwa wakati zikiwemo za jinai,rushwa kwa kuwa sisi kama mahakama pia tuko tayari katika kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda hivyo wananchi waendelee kuiamini mahakama” Alisisitiza Mhe. Prof. Juma.
Pia Mhe. Prof. Juma alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa mahakama kwa kufichua wale wachache wanaojihusisha na vitendo vya rushwa ili wachukuliwe hatua stahiki.
Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam yamekuwa kivutio kikubwa kwa wajasiriamali wa ndani na nje ya nchi ambapo makampuni zaidi ya 500 ya Tanzania yanashiriki na nchi 30 kutoka katika mabara mbalimbali hali inayochochea kukua kwa biashara kati ya Tanzania na Mataifa ya kigeni na pia kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda.