[caption id="attachment_21697" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelice Mafumiko akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima kutoka Kouvola nchini Finland Bi. Leena Kaivola wakati wa ziara yake katika Taaisisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na TEWW)
Samwel Gasuku- TEWW
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inatarajia Kushirikiana naTaasisi za Kimataifa katika Kukuza Kiwango cha Elimu hapa nchini, hasa elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii.
Akizungumza wakati wa ziara ya Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Kouvola cha nchini Finland Bi.Leena Kaivola aliyeongozana na baadhi viongozi waandamizi wa kituo hicho , MkurugenziwaTEWW Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa ushirikiano kati ya Taasisi yake na Kituo hicho unalenga kukuza Elimu na Utafiti ambao utakuwa na faida kwa pande zote mbili.
“Ushirikiano wetu unalenga kukuza kiwango cha elimu kupitia utaratibu wa kubadilishana uzoefu na kituo hiki cha Kouvola cha nchini Finland ambapo katika mazungmzo ya awali tumekubaliana kushirikiana kwa kipindi cha miaka mitano”Alisisitiza Dkt. Mafumiko.
Akifafanua Dkt. Mafumiko amesema dhamira ya Taasisi yake ni kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wa ndani na nje ya nchi katika kutoa fursa za elimu kwa vijana hasa wale waliopo nje ya shulena watu wazima kujipatia maarifa na ujuzi stahiki hapa nchini kwa kuwa sekta hiyo ni moja ya vipaumbele vya Serikali hasa katika kukuza maendeleo ya viwanda.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuuwa Kituo cha Kouvola Bi. Leena Kaivola amesema kuwa Kituo chake kitajikita katika kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza malengo ya pamoja yatakayoleta manufaa kwa pande zote mbili katika kukuza ushirikiano utakaoleta tija katika sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa Kituo chake kinatekeleza majukumu yanayofanana na yale yaTaasisi ya Elimu ya Watu wazima hali inayochochea kuwepo kwa ushirikianobaina yao.