Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Kuwa Mwenyeji Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama Kutoka Kusini na Mashariki Mwa Afrika
Sep 05, 2023
Tanzania Kuwa Mwenyeji Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama Kutoka Kusini na Mashariki Mwa Afrika
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu- Dodoma      

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma (kushoto) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim  Yonazi.       

Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe., Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi Wanachama wa Jukwaa hilo ni pamoja na Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe, Eswatini, Msumbiji, Seychelles, Botswana.

Nchi nyingine ni Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Jukumu la Mahakama za Nchi Wanachama katika Utatuzi wa Migogoro chini ya Utangamano wa eneo Huru la Biashara la Afrika: Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa kwa Ufanisi katika Utoaji Haki”.

Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wawakilishi wakifuatilia kikao kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi