Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Kukabidhiwa Uwenyekiti wa CILT Kanda ya Afrika
Mar 08, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29219" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Lojistiki na Uchukuzi Tanzania (CILT Tanzania), George Makuke (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya Tanzania kukabidhiwa uenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Lojistiki na Uchukuzi Kanda ya Afrika kwa miaka mitatu, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Ramadhan Sawaka na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Abraham Nyantori.[/caption]

Na Agness Moshi na Paschal Dotto-MAELEZO.

    Tanzania yawa Makamu wa Rais katika Taasisi ya Kimataifa ya Logistiki na Uchukuzi (CILT), ambayo itakabidhi Tanzania uwenyekiti wa taasisi hiyo, kwa  Kanda ya Afrika kwa miaka mitatu.

Makabidhiano hayo yatafanyika wakati wa Mkutano Mkuu ambao utaanza tarehe 14 mpaka 16 Machi 2018 na kukabidhiwa Uenyekiti wa CILT katika Jiji la Abuja nchini Nigeria.

[caption id="attachment_29220" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Lojistiki na Uchukuzi Tanzania (CILT Tanzania), Ramadhan Sawaka, akifafanua jambo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya Tanzania kukabidhiwa uenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Lojistiki na Uchukuzi Kanda ya Afrika kwa miaka mitatu, katikati ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo George Makuke na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Abraham Nyantori.[/caption]

Hayo yamesemwa na Rais wa Taasisi ya Logistiki na Uchukuzi Tanzania Bw. George Makuke alipoongea  na Waandishi wa Habari mapema leo, katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.

Makuke amesema kuwa, juhudi zilizoonyeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeifanya  CILT, itambulike kimataifa na kuonekana mfano bora kwa wengine.

“Utekelezaji wa miradi ya logistiki kama treni ya abiria kutoka kituo cha Stesheni kwenda Ubungo, Stesheni – Pugu,(TRC),  TAZARA mpaka Mwakanga na  mabasi ya mwendokasi (BRT) pamoja na miundombinu yake imechochea mafanikio hayo” Amesema Makuke.

[caption id="attachment_29221" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Lojistiki na Uchukuzi Tanzania (CILT Tanzania), George Makuke (kulia) akimkabidhi tuzo Cyprian Moses kwa kufanya vizuri katika mafanikio ya usafirishaji wa anga kwa vijana wanaochipukia, Katikati ni Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Ramadhan Sawaka.[/caption] [caption id="attachment_29222" align="aligncenter" width="945"] Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Lojistiki na Uchukuzi Tanzania (CILT Tanzania), George Makuke (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya Tanzania kukabidhiwa uenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Lojistiki na Uchukuzi Kanda ya Afrika kwa miaka mitatu.
Picha na Eliphace Marwa -MAELEZO[/caption]

Aidha, Tanzania hatujapata nafasi ya uenyekiti kutokana na utaratibu wa zamu ,ila kutokana na  vigezo vya ubunifu, ufanisi na juhudi za Serikali kwa kipindi cha miaka ya mitano iliyopita, katika kuboresha logistiki na uchukuzi ndio maana tumepata nafasi hiyo.

Akitoa ufafanuzi Makuke amesema nafasi hiyo itawawezesha kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali, Sekta hizo ni pamoja na  Utalii, Ujenzi wa Miundombinu, Kuimarisha habari na utamaduni (lugha ya Kiswahili), uchukuziu na mawasiliano.

Naye Katibu Mtendaji wa CILT Ramadhani Sawaka aliongeza, nafasi hiyo imewapa  fursa Tanzania   kuwa wenyeji wa mkutano wa CILT kanda ya Afrika utakofanyika Zanzibari Aprili 2019. Ambapo, utakaohudhuriwa na wajumbe washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Zambia, Ghana, Zimbabwe na Afrika Kusini.

 “Kuelekea uchumi wa viwanda taasisi yetu imejikita katika mambo makuu mawili ambayo  ni kutoa ushauri wa logistiki na uchukuzi na kuendeleza taaluma itakayowasaidia watu kuendelea kwani maendeleo ya watu ndio maendeleo ya nchi”, Alisisitiza Sawaka.

Tasisi hiyo iko chini ya Malkia wa Uingereza ikijumlisha nchi 34 duniani na inawanachama wapatao elfu 34. Ambavyo Tanzania ina wanachama  660 na makampuni wanachama 40 yakiwemo Zakaria HansPoppe , Said Salim Bakhresa, kampuni ya ASAS, na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi