Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Ina Ziada ya Tani 3,013,515 ya Mazao ya Chakula Hasunga
Jan 02, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39367" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma tarehe 2 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)[/caption]  
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
 
Kwa mliganisho wa mahitaji na uzalishaji nchi ina ziada ya tani 3,013,515 na imejitosheleza kwa asilimia 123 na 120 mtawalia ambapo uzalishaji katika msimu wa 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa tani 15,900,864 na 16,172,841 mtawalia ambapo mahitaji ya chakula yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 13,159,326, na 13,300,034 kwa mwaka wa ulaji 2017/2018 na 2016/2017 mtawalia.
Uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa uzalishaji wa 2017/2018 ulifikia tani 16,981,974 zikiwemo tani tani 9,537,857 za mazao ya nafaka na tani 7,354,117 mazao yasiyo nafaka, kiwango ambacho kimeiwezesha nchi kutosheleza mahitaji yake ya chakula ya tani 13,569,285 katika mwaka 2018/2019 kwa kiwango cha utoshelevu (Self Sufficiency Ratio-SSR) cha asilimia 124.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 2 Januari 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma.
Alisema Uzalishaji wa mahindi katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 6,273,150; 6,680,758 na 6,148,699 mtawalia,wakati mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 5,462,390; 5,407,499 na 5,202,405 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017, Ambapo ziada ya tani 810,760(2018/2019); 1,273,259(2017/2018)  na 946,284(2016/2017) zilipatikana.
Uzalishaji wa mchele katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 2,219,628; 1,593,609; na 2,229,071 mtawalia,mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 990,044; 924,435; na 976,925 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017,Ziada ya tani 1,229,583(2018/2019); 669,175(2017/2018) na 1,252,146(2016/2017) zilipatikana.
Mhe Hasunga alisema kuwa kutokana na ziada hizo za uzalishaji nchi imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi jirani. Kwa mfano, kulingana na takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika kipindi cha mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018 jumla ya tani 64,477.95 za Mahindi zenye thamani ya shillingi billioni 90.6 na Maharage tani 99,434.45 zenye thamani ya shillingi bilioni 222.0 ziliuzwa katika nchi za DRC, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini na Uarabuni.
Hasunga aliongeza kuwa Kati ya mwaka 2015/2016 na 2017/2018 uzalishaji wa mazao ya Asili ya Biashara umeongezeka kwa viwango tofauti tofauti, ambapo zao la korosho kwa sasa linalimwa katika mikoa 17 na Halmashauri 90 hapa nchini baada ya kuanza kwa mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao la korosho mnamo mwaka 2013/2014 kupitia uhamasishaji wa kilimo hicho katika mikoa mipya. 
Amesema kuwa Mikoa ya asili inayoongoza kwa kilimo cha zao la korosho ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga. Katika miaka ya hivi karibuni mikoa mingine mitano nayo imeanza kuzalisha korosho kwa kiasi kidogo ambayo ni Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Njombe.
Alisema kuwa taarifa ya uhakiki na malipo kwa wakulima mpaka kufikia tarehe 29 Desemba 2018 tayari Vyama vilivyohakikiwa na kulipwa ni 450.
Malipo yaliyohakikiwa na kuwasilishwa benki ni tsh 231,937,341,674, Malipo yaliyolipwa katika akaunti za Wakulima ni tsh 210,485,753,571, Korosho iliyolipiwa ni Kilo 70,284,043, Kiasi cha Korosho iliyokusanywa katika maghala makuu ni Tani 195,175.844, na Kiasi cha Korosho iliyosombwa na kupelekwa katika maghala ya Hifadhi ni Tani 35,175.844
Katika taarifa yake na waandishi wa habari Mhe Hasunga ameeleza kuwamatumizi ya mbegu bora za pamba yameongezeka kutoka tani 14,500mwaka 2015/2016 hadi tani 18,500 mwaka 2017/2018 na matarajio ni kufikia tani 25,000 msimu wa 2018/2019. Mpaka sasa kiasi cha mbegu tani 27,769 zimesambazwa na ni asilimia 37 zaidi ya kiasi kilichoombwa na Wilayaambacho kilikuwa tani 20,284.
Aidha, Uzalishaji wa chai kavu umeongezeka kutoka tani 32,628 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 34,010 mwaka 2017/2018. Matumizi ya mfumo wa ushirika umeongeza bei ya kilo moja ya majani mabichi kutoka wastani wa Shilingi 251 mwaka 2015/16 hadi  shilingi 314 mwaka 2017/18. Thamani ya mauzo ya chai nje ya nchi imeongezeka kutoka Dola za kimarekani51,794,854.00 mwaka 2015/2016 hadi kufikia Dola za kimarekani62,167,167.00 mwaka 2017/2018.
Kuhusu zao la Mkonge uzalishaji umeongezeka kutoka tani 39,393 mwaka 2015/16 hadi tani 43,279 mwaka 2017/18. Bei ya tani moja ya Katani daraja la UG mwaka 2015/2016 ilikuwa Shilingi 2,200,000 na mwaka 2017/2018 imefikia Shilingi 3,330,000 sawa na asilimia 50. Thamani ya mauzo ya singa nje ya nchi ni kutoka dola za Kimarekani 35,991,161 mwaka 2015/16 hadi dola za Kimarekani 45,835,845 mwaka 2017/18.
Akieleza kuhusu zao la Sukari Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali imeimarisha udhibiti wa uingizaji holela wa sukari kutoka nje hali iliyoimarisha soko la sukari nchini.
Udhibiti huo umechochea ongezeko la uzalishaji wa sukari kutoka tani 293,075 mwaka 2015/2016 hadi takriban tani 307,431.14 mwaka 2017/2018. Aidha, uzalishaji wa sukari unatarajiwa kuongezeka na kufikia tani 352,600 mwaka 2018/2019. 
 
Vilevile, Serikali imeratibu uanzishwaji wa mashamba mapya ya miwa ya Mkulazi I (Ngerengere), Mkulazi II (Mbigiri) na Shamba la Bakhresa -Bagamoyo Sugar (Makurunge).  Sekta ya Sukari kwa ujumla inatoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa watu 57,000 pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa watu wengine takriban 75,000 ambao wanahusika na shughuli zinazotoa huduma kwenye mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa sukari nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi