Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania, China Kuimarisha Soko la Bidhaa za Kilimo
Jan 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27845" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Charles Tizeba akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao baina yake na Naibu Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Dkt. Qu Dongyu (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo wa Tanzania Dkt. Mary Mwanjelwa. (Picha na Frank Shija - MAELEZO)[/caption]

Na. Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amekutana na Naibu Waziri wa Kilimo China, Dkt. Qu Dongyu na kukubaliana kushirikiana kuwasaidia wakulima wa Tanzania kulima mazao kwa kuzingatia ubora unaohitajika kwa ajili ya soko la bidhaa za kilimo nchini China.

Dkt. Tizeba ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam ya kumalizika kwa kikao baina ya Mawaziri kujadili njia bora ya kuwasaidia wakulima kuwa na soko la uhakika nchini China.

“Tumekubaliana kuunda kikosi kazi cha wataalam wa nchi hizi mbili kuangalia kwa undani jinsi ya kuboresha kilimo chetu hasa katika suala la masoko kwani wakulima wetu wanazalisha bila kuwa na soko hivyo mkakati uliopo ni wa kuwaleta wawekezaji kutoka China kuingia mkataba na wakulima wa Tanzania na kuwaelekeza vigezo vya uzalishaji wanaoutaka ili wakizalisha wawe na uhakika na soko.”amesema Dkt. Tizeba.

Ameongeza kuwa katika kikao hicho imekubalika kuwa wawekezaji wa China waeleze kwa uwazi na kujaili vigezo vya baadhi ya mazao ili Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Marry Mwanjelwa atakapokwenda China mwezi Mei mwaka huu, akutane na wawekezaji mbalimbali watakaokuja kuwekeza nchini wakiwa na uhakika wa kuzalisha kwa ubora wanaouhitaji ikiwa ni moja ya ushirikiano wa kitaalam kati ya nchi hizo.

[caption id="attachment_27846" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Charles Tizeba akichangia hoja wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu ushirikiano katika sekta ya kilimo na ujumbe kutoka Serikali ya China ukiongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Dkt. Qu Dongyu (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bibi. Jacqeline Mboya (Picha na Frank Shija - MAELEZO)[/caption]

Vile vile Dkt. Tizeba amesema kuwa ni lazima kupata fursa ya kutangaza mazao ya Tanzania nchini China hivyo katika majadiliano hayo Serikali ya China imekubali kutoa nafasi ya kuwa na maonesho ya kudumu ya bidhaa za Tanzania nchini mwao.

Akiongelea kuhusu usindikaji wa mazao, Dkt Tizeba amesema kuwa uzalishaji wa mazao ni mkubwa lakini mengi yanaharibika kwa kutokuwa na viwanda vya kusindika kwa hiyo uhifadhi wa mazao kuanzia shambani hadi sokoni unatakiwa uwe wa uhakika hivyo tunawakaribisha watu wa China kuja kuwekeza katika viwanda vya usindikaji wa mazao.

[caption id="attachment_27847" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Dkt. Qu Dongyu akichangia hoja wakati wa kikao cha majadiliano na ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba (hayupo pichani) kuhusu ushirikiano katika sekta ya hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapa nchini Mhe. Mhe. Wang Ke na Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Lin Zhiyong (Picha na Frank Shija - MAELEZO).[/caption]

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo China, Dkt. Qu Dongyu amesema kuwa nchi hizo mbili zina urafiki wa muda mrefu hivyo Serikali ya China imejidhatiti kusaidiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo yakiwemo ya uwekezaji, teknolojia, kujengea uwezo wananchi pamoja na ukuzaji wa soko.

“Soko la China ni kubwa na Tanzania ina vitu vingi vya kupeleka katika soko letu hivyo tunahitaji wakulima wengi kuleta mazao nchini kwetu, kwa kuzingatia hilo tutahakikisha wakulima wa Tanzania wanaweka juhudi na maarifa katika kilimo pamoja na kushirikiana na wawekezaji wetu ili kufahamu vigezo vya mazao tunayoyahitaji kabla ya kulima,” amesema Dkt. Qu Dongyu.

Kikao hicho ni muendelezo wa mazungumzo yaliyojadiliwa na Marais wa Tanzania na China katika kuboresha kilimo hivyo kikao cha leo kimefanyika kwa ajili ya kuweka mipango ya utekelezaji wa makubaliano na maelekezo ya Marais hao.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi