[caption id="attachment_36870" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Aggrey Mwanri (katikati) ili naye amkaribishe Naibu Waziri wa Ujenzi Elias John Kwandikwa (kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na Menejimenti ya Mkoa huo alipopita Tabora akiwa safarini kwenda Mkoani Shinyanga jana.[/caption]
Na Tiganya Vincent - RS Tabora
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Wakala wa Barabara wa Tanzania mkoani Tabora kuangalia uwezekano wa kubadilisha mfumo wa taa za barabarani mkoani humo kutoka matumizi ya umeme wa TANESCO na kuanza kutumia umeme wa jua ili kupunguza gharama za uendeshaji kila mwezi.
Kauli hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias John Kwandikwa jana mkoani Tabora apokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Shinyanga.
Alisema kuwa pamoja na gharama za kubadilisha taa hizo kutoka matumizi ya umeme wa TANESCO kwenda matumizi kuwa kubwa mwanzo lakini manufaa yake ni makubwa.
[caption id="attachment_36871" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akitoa salamu za Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias John Kwandikwa (kushoto) aliyepita Mkoani humo wakati akielekea Mkoani Shiinyanga jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu.[/caption]Naibu Waziri huyo alisema za barabarani muhumu katika kuimarisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao katika mitaa mbalimbali nyakati za usiku.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kwa muda mrefu taa hizo zimekuwa haziwaki kwa sababu ya kuwepo na mvutano juu ya nani kati Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na TANROADS Mkoa huo anayepaswa kulipia ankra za matumizi ya umeme katika barabara kuu.
Alimwomba Naibu Waziri huyo kusaidia kutatua tatizo hilo kwa kuwaagiza TANROADS wawasaidie kubadilisha taa hizo ili ziweze kusaidia katika kuimarisha usalama mitaani.
[caption id="attachment_36873" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (kushoto) akibadilisha mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wa pili kutoka kushoto), Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (wa pili kutoka kulia) na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora Damiani Ndabalinze(kulia) wakati alipopita mkoani humo jana akiwa safarini kuelekea Shinyanga.[/caption]Kwa upande wa Meneja wa Tanroads mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze alisema kuwa barabra hiyo ina jumla ya nguzo 97 na gharama za uendeshaji wa taa kwa mwezi mmoja hivi sasa kwa kutumia umeme wa TANESCO ni milioni 2 .
Barabara za kutoka Tabora kwenda Urambo imewekwa taa za barabarani lakini zimekuwa haziwaki kwa sababu ya gharama kubwa za ankra zinaletwa na TANESCO.