TANGAZO KWA WADAIWA SUGU WA MADENI YA PROGRAMU YA “COMMODITY IMPORT SUPPORT (CIS) NAFOOD AID COUNTERPART FUND (FACF)” Wizara ya Fedha na Mipango inawataka wadaiwa sugu wa madeni ya Commodity Import Suport (CIS)na FACF, walipe madeni yao mara moja. Madeni haya ni mkopo wenye masharti nafuu yaliyotolewa kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara, ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha Miezi 18 tangu walipopewa mikopo hiyo. Kwa mujibu wa sheria ya CIS (The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R. E. 2002 (s.8 (1)(b), Mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asimilia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali katika kipindi husika. Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu. Serikali inatangaza kwa mara ya Mwisho kufuatia baadhi ya wadaiwa ambao wameshindwa kuitikia wito wa matangazo ya awali ya tarehe 30/12/2015 na 05/04/2018. Hatua za kisheria zitachukuliwa mara baada ya kutoka kwa tangazo hili. ORODHA YA KWANZA YA WADAIWA SUGU WA MADENI YATOKANAYO COMMODITY IMPORT SUPPORT(CIS) NA FOOD AID COUNTERPART FUND (FACF).