Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tamasha la Kizimkazi Kuinua Uchumi Unguja
Aug 31, 2023
Tamasha la Kizimkazi Kuinua Uchumi Unguja
Shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) lililofanyika Paje, Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.
Na Mwandishi Wetu

Tamasha la Kimkazi linalofanyika kila mwaka mkoani Kusini Unguja, ambalo limeasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kijijini kwake Kizimkazi miaka nane iliyopita, limekuja na sura mpya ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo mkoani humo.

Ambapo lengo la kuanzishwa kwa tamasha hilo linaloendelea kukua mwaka hadi mwaka linatajwa kuwa ni kudumisha mila na desturi za wakazi wa Kizimkazi na kwa mara ya kwanza limefanyika katika Kata ya Paje, wilayani Kusini.

Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Kusini, Bw. Othman Abdallah amesema tamasha hilo ni kichocheo kikubwa cha uchumi wilayani humo, kupitia miradi mbalimbali inayozinduliwa katika tamasha hilo.

Bw. Othman amesema “Ni ndoto ya Mhe. Rais kuona tamasha hili linakua mpaka kufikia ngazi ya kimataifa ambapo pia litatangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana Tanzania pamoja na kudumisha na kutangaza mila na desturi zetu”.

Anafafanua “Katika tamasha la mwaka huu Mhe. Rais anazindua miradi mbalimbali ikiwemo, ujenzi wa ukumbi wa mikutano na jengo la madarasa katika Shule ya Muyuni B na kuweka mawe ya msingi katika Shule ya Maandalizi Tasani na Kiwanja cha Kufurahisha Watoto pamoja na kukabidhi magari mawili katika Kituo cha Polisi Kizimka Mkunguni”.

Vilevile Mhe. Rais amezindua hoteli ya hadhi ya Nyota Tano, Kwanza Resort iliyopo Kizimkazi ambayo imetoa ajira kwa watu 300 kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na matawi mapya ya benki za NMB na PBZ katika kata ya Paje.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi