Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.
Mtaalamu kutoka Taasisi ya Africa Regional Manager, Global Partnership for Sustainable Development Data Bw. Davis Adieno akiwasilisha mada katika Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma ikiratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshighulikia Usawa wa Kijinsia wa Wanawake (UN Women) Bibi Usu Mallya akizungumzia maana ya takwimu za kijinsia wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.
Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bw. Said Ameir wakati wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.
Mratibu wa Mpango Kabambe wa kuboresha na kuimarisha Takwimu Nchini (Tanzania Statical Master Plan ) Bw. Philemon Mahimbo akiwasilisha mada wakati wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu, Usawa wa Kijinsia, Utawala, Amani na Usalama leo Jijjini Dodoma.
Na Mwandishi wetu
Warsha ya Wadau Kuhusu hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na Amani .
Akizungumza wakati wa warsha ya siku mbili Leo Mjini Dodoma Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja amesema kuwa warsha hiyo ni muhimu na itasaidia katika kubainisha maeneo yanayotakiwa kufanyiwa tafiti na kuzalisha takwimu zitakazotumika katika kuchochea maendeleo mara baada ya kubaini maeneo ambayo bado takwimu zake hazijakusanywa.
" Warsha hii itatusaidia kuona ni wapi kuna takwimu ambazo hazijafikiwa kweye maeneo mbalimbali ya kisekta ili ziweze kukusanywa na kusaidia katika kuleta maendeleo" Alilisisitiza Bibi Ruth.
Akifafanua amesema kuwa jukumu kubwa la Ofisi hiyo ni kukusanya na kuchambua na hatimaye kutoa takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo .
Kwa upande wake mmoja wa wawezeshaji katika warsha hiyo Davis Adieno kutoka nchini Kenya amesema kuwa wanapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwa na warsha hiyo ya wadau kwa kuwa itasaidia takwimu zinazokusanywa zitasaidia wadau katika kupanga mipango ya maendeleo.
Aliongeza kuwa wadau wamekusanyika katika warsha hiyo ili kujifunza na wataweza kushiriki kikamilifu katika kuondoa umasikini.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Usawa wa Kijinsia wa wanawake ( UN Women) Bibi Usu Mallya amesema kuwa uchambuzi wa Takwimu unasaidia kuonesha upungufu wa takwimu zinazotakiwa kukusanywa katika sekta mbalimbali.
Aliendelea kusema kuwa Takwimu zilizopo zimenyumbulishwa kijinsia na kupitia warsha hiyo washiriki wataweza kuendeleza takwimu za kijinsia.
Warsha ya ya Wadau Kuhusu hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na Amani inafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili ikiwashirikisha wadau kutoka sekta ya umma , Binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo.