Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB Yatoa Tshs Bilioni Mbili Kuendeleza Miradi ya Miwa na Mpunga Kilombero
Aug 20, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_9531" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.[/caption]

Na: Said Mkabakuri, TADB

Wakulima wa Kilombero wapata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wa jumla ya shilingi bilioni mbili ili, kuendeleza miradi ya kilimo cha miwa na mpunga.

Akizungumza wakati wa kukagua miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw Fransis Assenga amesema; “ nimeridhishwa na maendeleo ya miradi hii, ambayo inachochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini”

[caption id="attachment_9532" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo.[/caption] [caption id="attachment_9535" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Afisa Tarafa ya Mang’ula, Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Kilimo Shadidi kinachofanyika katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati). Wengine wanaosikiliza na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.[/caption]

Aidha, Bw Assenga amewasihi wakulima hao kutumia vema mikopo hiyo, ili kujiletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. James Ihunyo  aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.

[caption id="attachment_9538" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege (kushoto) akiongea na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ulioambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kulia). Benki ya Kilimo ilifanya ya ukaguzi wa miradi iliyopatiwa mikopo ili kujionea maendeleo ya miradi wilayani Kilombero.[/caption] [caption id="attachment_9544" align="aligncenter" width="750"] Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.[/caption]

“Lengo la kuwapa mikopo ni ili kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha kulipa mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” amesema Ihunyo.

Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi