Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB Yajitosheleza Kimtaji – Kaimu Mkurugenzi
Aug 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34673" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Benki hiyo mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila kuwasilisha taarifa ya utendaji ya Benki hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi wetu,

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine amesema kuwa TADB ina mtaji wa kutosha kwa sasa kwa ajili ya kuwahudumia wakulima.

Bw. Justine alikuwa akizungumza na wanahabari kwa nia ya kutoa taarifa za ziada juu ya mtaji wa benki hiyo.

Bw. Justine alisema kuwa kwa mujibu wa upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2011 wakati wa mchakato wa kuianzisha TADB, ilibainika kwamba mtaji unaohitajika kwa ajili ya kuiwezesha TADB ifikie malengo yake ya kimkakati na kutimiza matarajio ya Serikali na Wakulima ifikapo mwaka wa 2035, ilikuwa Dola za Marekani Milioni Mia Tano (US$ 500 milioni) ambazo zilikuwa sawa na Tsh bilioni 800 (Authorized Capital – Mtaji halisi).

Kwa mujibu wa Bw. Justine, tangu kuanza shughuli rasmi za ukopeshaji mwaka 2015, Serikali imekuwa ikiendelea kuipatia Benki hiyo mtaji. Mwaka 2015, Serikali iliweka mtaji wa Sh. bilioni 60 (paid-up share capital – mtaji lipwa); mwaka 2017 Serikali ili iwezesha benki kupata mkopo wa muda mrefu kutoka Benki ya Maendelea ya Africa (AfDB) ambapo awamu ya kwanza mkopo huo benki ilipatiwa mkopo wa wa TSh. bilion 104. Awamu ya pili ikitarajiwa mwanzoni mwa mwaka 2019.

“Kwa hiyo kwa sasa Benki ina mtaji wa kutosha kwa ajili ya kukopesha wakulima nchini,” alisema.

Kaimu Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mpaka kufikia mwisho wa mwezi wa Julai mwaka huu, Benki ya Kilimo imefanikiwa kutoa mikopo inayofikia kiasi cha zaidi Sh bilioni 48.6 ikiwa ni ukuaji wa shilingi bilioni 37.2 katika kipindi cha miezi saba ya mwaka 2018.

“Katika kutimiza maelekezo ya Serikali ndani ya kipindi cha miezi saba ya mwaka 2018, Benki imefanikiwa kukopesha kiasi cha shilingi bilioni 37.2 kati ya shilingi bilioni 48.6 zilizotumika kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo kupitia mnyororo mzima wa ongezeko la thamani,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Justine mikopo hii imeweza kuwanufaisha zaidi ya wakulima 520,291 ikiwa na lengo la kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara nchini.

Bw. Justine aliongeza Benki ya Kilimo inatekeleza kwa vitendo maelekezo ya Serikali ya awamu ya tano ya kusaidia kukabiliana na upungufu wa mikopo ya gharama nafuu kwa wakulima nchini kwa kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika  sekta ya kilimo nchini.

“Nawakaribisha wakulima watanzania kufika kwenye benki yao kupata na kufaidi na huduma zao. Benki hii ni ya wakulima na wao ndo wataikuza kwa kuendelea kutumia huduma za benki hii” alisema Bw. Justine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi