Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taasisi ya ICHIP Kutoka Nchini Marekani Kushirikiana na Ofisi ya Hakimiliki Tanzania
Nov 30, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Anitha Jonas - OFISI YA HAKIMILIKI Dar es Salaam.


Mtaalamu na Mshauri wa Mifumo ya Udukuzi na Miliki Ubunifu (International Computer Hacking and Intellectual Property -ICHIP) na Mshauri wa Sheria kutoka Idara ya Haki na nchini Marekani (USDOJ) na Jeremy  Beck  Afisa Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania leo Novemba 29, 2022 wametembelea Ofisi ya Hakimiliki Tanzania na  kufanya mazungumzo na Msimamizi wa Hakimiliki, Doreen Anthony Sinare.


Katika mazungumzo hayo, Tanya amesema amekuja nchini Tanzania Kwa ajili ya  maandalizi ya kazi ya Kamati "Africa Regional  IP bench book working committee" inayolenga kuongeza uelewa wa masuala ya Miliki Ubunifu lakini pia kufahamu utekelezaji wa masuala ya Miliki Ubunifu nchini Tanzania. Pamoja na hayo alipenda kufahamu jinsi Ofisi yake inavyoweza kushirikiana na Ofisi za Miliki Ubunifu na usimamizi wa haki kwa Mahakama na waendesha mashitaka nchini Tanzania. 


Tanya ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa Mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki yaliyofanyika hivi karibuni na pia ameipongeza Ofisi ya Hakimiliki kwa namna inashirikiana na mashirika ya Kimataifa katika usimamizi wa hakimiliki. Amekiri kuwa safari ya leo itaongeza ushirikiano kati ya pande mbili.


"Nimefurahi sana kufika COSOTA na natumaini tutaendelea kushirikiana zaidi katika kutoa elimu ya hakimiliki na kujenga uwezo masuala ya hakimiliki kwa wadau," alisema Tanya.


Nae Msimamizi wa Hakimiliki, Doreen Anthony Sinare alieleza kuwa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) na Shirika la Miliki bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) na CISAC kwa sasa wanasubiri kanuni mpya zisainiwe ili waweze kusaidia kutoa elimu ya namna ya kuanzisha na kusimamia Kampuni ya Ukusanyaji na Ugawaji wa Mirabaha (CMO).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi