Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa Kwa Umma.
May 31, 2017
Na Msemaji Mkuu

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

31 Mei, 2017

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi