KUAHIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwatangazia Vyama vya Siasa na umma kwa ujumla kuwa kikao na Semina ya Baraza la vyama vya Siasa vilivyokuwa vifanyike siku ya tarehe 21 na 22 Desemba 2017, Jijini Dar es salaam vimeahirishwa hadi hapo tarehe nyingine itakapopangwa.
Kikao hicho kimehirishwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa Vyama vya Siasa na wadau wa Vyama vya Siasa kushiriki katika shughuli za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika 13 January 2018. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Jacqueline Kilama
Kny. MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
19 Disemba, 2017