JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS, IKULU, 1 BARABARA YA BARACK OBAMA, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Oktoba, 2017 amewasili Zanzibar ambapo keshokutwa tarehe 14 Oktoba atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya siku ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kilele cha wiki ya vijana kitaifa zitakazofanyika katika uwanja wa Amaan.
Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli ametua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Zanzibar
12 Oktoba, 2017