Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Feb 07, 2019
Na Msemaji Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Februari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe ambaye ni Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji, Mazingira na Makazi Vijijini Mhe. Pretence Shiri.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Shiri amekabidhi barua kutoka kwa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa.

Mhe. Shiri ameishukuru Tanzania kwa mchango mkubwa ilioutoa kwa Zimbabwe wakati wa kupigania uhuru uliopatikana mwaka 1980, na amebainisha kuwa Wazimbabwe wanaichukulia Tanzania kuwa ni nyumbani.

“Tunafurahi sana kuwa hapa Tanzania, tunajisikia ni nyumbani kwetu, bila Tanzania Zimbabwe isingepata uhuru mwaka 1980, ingechukua muda mrefu sana, lakini tunafurahi kuwa Watanzania walijitolea kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Zimbabwe inakuwa nchi huru” amesema Mhe. Shiri.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Bw. Charles Stuart na baada ya mazungumzo hayo Bw. Stuart amesema mazungumzo baina yao yalikuwa mazuri na yamehusu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Umoja wa Ulaya na dhamira ya umoja huo kuisadia Tanzania.

“Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umekuwa imara siku zote, na kumekuwa na maeneo mengi ya uhusiano yenye maslahi muhimu kwa pande zote na kwa miaka mingi” amesema Mhe. Stuart.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

07 Februari, 20

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi