Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Lut Jen. Mstaafu Samweli A. Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mzinga.
Lut Jen. Mstaafu Ndomba anachukua nafasi ya Bw. Andrew Severin Nyumayo ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huohuo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Zacharia M.D. Mganilwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwakipindikingine cha miakamitano.
Uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 05 Novemba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano yaRais, IKULU
Dar es Salaam
07 Novemba, 2018