Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. January Henry Msofe kuwa Mwenyekiti waTume ya Kurekebisha Sheria.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewateua Bw. Iddi Mandina Bw. Julius Kalolo Bundala kuwa Makamishna wa muda waTume ya Kurekebisha Sheria.
Wakati huohuo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Paul Kimiti kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi zaTaifa (NARCO).
Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 14 Oktoba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
16 Oktoba, 2018