Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Dalmas Lucas Nyaoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Dkt. Nyaoro ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anachukua nafasi ya Bi. Hawa Magogo Mmanga ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi wa Dkt. Nyaoro umeanza tarehe 10 Oktoba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Oktoba, 2018