Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Aug 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA FOCAC

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Ijumaa, Oktoba 31, 2018) kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

IJUMAA, OKTOBA 31, 2018.

 
   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi