Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa leo tarehe 29 Juni, 2018 amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali hapa nchini na kurejea nchini kwake Zimbabwe.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Mnangagwa ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Kabla ya kuondoka nchini Mhe. Rais Mnangagwa ametembelea chuo cha kilimo na mifugo cha Kaole kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani ambacho mwaka 1963 kilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa chama cha FRELIMO, na yeye akiwa mmoja wa waanzilishi wa kambi hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
29 Juni, 2018