Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Al-Balsam la nchini Saudi Arabia itakuwa na kambi maalum ya matibabu ya kusaidia wagonjwa wa moyo ambao mishipa yao ya damu haipitishi damu vizuri na inahitaji kuzibuliwa kwa kuwekewa kifaa kiitwacho Stent.
Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo hayo ili waweze kufanyiwa matibabu. Wagonjwa wafike Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete tarehe 26/09/2018 kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ambayo yataanza tarehe 29/09/2018 hadi tarehe 05/10/2018.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo: 022-2151379,0782-042019,0713-236502,0713-607183,0754-870969 na 0788-465169 ili uelekezwe utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/09/2018