Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shule Zote Nchini Kufunguliwa Juni 29, 2020
Jun 16, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53250" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia leo Jijini Dodoma, wakati wa shughuli za kuvunja Bunge la kumi na moja zilizofanyika Bungeni jijini Dodoma. [/caption]

Jonas Kamaleki, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kufungua shule zote nchini  kuanzia Juni  29, 2020 ikiwa ni pamoja na  kuendelea kwa shughuli mbalimbali  baada ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19)  kupungua sana nchini.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akihutubia Bunge la 11 ambalo limemaliza muda wake wa kipindi cha miaka mitano tangu Novemba 2015.

 “Tarehe 29 Juni 2020 itakuwa Jumatatu hivyo shule zote ziendelee na masomo pamoja na shughuli nyingine ziendelee, tumewachelewesha watu kufunga ndoa,” alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa Serikali imechukua tahadhari kupambana na Corona ikiwemo kumtanguliza Mungu ambaye amejibu maombi ya watanzania, hivyo aliwashukuruviongozi mbalimbali wa dini wakiwemo Wachungaji, Maaskofu na Mashehe.

Kutokana na hatua zilichokuliwa ikiwemo kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea kama kawaida wakati wa kipindi cha mlipuko wa Corona, uchumi wa Tanzania hautaathirika sana tofauti na nchi nyingine.

Shule hizo zilifungwa Aprili 17, 2020 ikiwa ni moja ya tahadhari katika kupunguza maambukizi ya Corona kwa tamko lililototelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliainisha mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kuboresha elimu, utoaji wa huduma za afya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, madaraja na viwanja vya ndege. Vile vile alitaja mafanikio mengine kuwa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika, kupambana na rushwa, dawa za kulevya, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kusimamia mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini, kujenga viwanda na kuongeza ajira nchini.

Aidha, Rais Magufuli alikemea dhana ya kupinga kila kitu kinachofanywa na Serikali akisema kuwa hilo sio jambo jema. Amewataka watanzania kuendelea kuchapa kazi ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuiletea Tanzania maendeleo.

Bunge hilo,  Rais Magufuli alilizindua Novemba 20, 2015 na kulifunga leo (Juni 16, 2020) baada ya kudumu kwa miaka mitano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi