Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shule Aliyosema Nyerere Yaendelea Kutengeneza Wazalendo
Oct 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Lilian Lundo - Tabora

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Tabora, Deogratius Mwambuzi amesema kufundisha shule hiyo kwa miaka 20 kumemfanya kuyaishi maisha ya Hayati Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu Mwambuzi amesema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii, yaliyofanyika shuleni hapo Oktoba 13, 2014.

"Namshukuru Mungu kwa kujifunza uzalendo, na kwa kuishi yale mambo ambayo Baba wa Taifa alikuwa akiyasisitiza na kuyazungumza. Najiona kuwa mzalendo kamili wa nchi yangu," alisema Mwalimu Mwambuzi.

Aliendelea kusema kuwa, Baba wa Taifa aliamua kuifanya shule ile kuwa shule ya kuandaa viongozi katika nyanja ya ulinzi na usalama wa nchi. Vilevile amesema shule hiyo ya kihistoria inaandaa wakombozi wa Taifa la Tanzania.

"Shule hii ilianzishwa kwa lengo kubwa la kuandaa viongozi wa kuja kulikomboa Taifa hili, tokea enzi ya ukoloni na baada ya kupata Uhuru wa Tanganyika 1961," alifafanua Mwalimu Mwambuzi.

Wanafunzi wa shule hiyo wengi wao wamekuwa wakiishi maisha ya Hayati Nyerere kutokana na shule hiyo kuzungukwa na kumbukumbu mbalimbali za Nyerere, ikiwa pamoja na ramani ambayo inaonyesha matukio mbalimbali aliyoyafanya Mwalimu Nyerere tangu anazaliwa mpaka kupata Uhuru mwaka 1961.

Kumbukumbu nyingine ni nukuu za Mwalimu Nyerere ambazo zimepamba kuta mbalimbali za shule hiyo, moja ya nukuu hizo inasema "nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote".

Aidha, nukuu hizo zimekuwa ni chachu kwa wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii ili baadae waje kuwa viongozi wakubwa wa nchi na kuiletea nchi mafanikio kama ambavyo walifanya viongozi wengine waliosoma shuleni hapo, akiwepo Baba wa Taifa na Waziri Mkuu wa Pili wa Tanganyika, Rashid Mfaume Kawawa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi