[caption id="attachment_33815" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (katikati) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu Mkoa wa Songwe (hawapo picha) wakati alipokuwa akifunga warsha ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau hao yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania leo Mjini Vwawa, Wilayani Mbozi,kutoka kushoto ni Katibu Mtendi Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw. Juma Mhina.[/caption]
Na: Anitha Jonas – WHUSM,Vwawa – Mbozi
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka waandaji wa kazi za filamu mkoa wa Songwe kutumia mandhari za mkoa huo na vivutio vya kiutalii vilivyopo katika mkoa huo kuandaa filamu za kiutamaduni na zile zinazotangaza vivutio vilivyopo katika mkoa huo.
Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hilo leo Mjini Vwawa Wilayani Mbozi alipokuwa akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu katika mkoa huo yaliyoandaliwa na bodi ya filamu Tanzania.
[caption id="attachment_33816" align="aligncenter" width="750"]“Mkoa wa Songwe umebarikiwa kwa kuwa na vivutio vyingi vya kiutalii na mandhari nzuri pamoja na kimondo ambacho ni kivutio cha kipekee hivo ni vyema tujifunze kuenzi vya kwetu kama na kuigiza vitu vilivyoko katika mazingira yetu mambo ya kiutamaduni badala ya kuigiza mambo yaliyoko nje ya Mkoa wetu tusiyo na ufahamu mzuri juu yake,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe hizo za kufunga warsha hiyo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wadau hao wa sekta ya filamu wa mkoa huu kuzingatia maadili katika unandaaji wa kazi zao za filamu kwani serikali inafuatilia kwa kaziru suala la maadili na kwa kazi yoyote ya filamu inayokuwa imevuka mipaka katika maadili ya kitanzania basi itachukuliwa hatua stahiki.
[caption id="attachment_33817" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wa Katibu wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa mara baada ya kuhitimisha warsha hiyo Bodi ya Filamu Tanzania ilifanya maadhimio kadhaa na wadau hao ikiwemo azimio la kuwataka wadau hao kuhuwisha uongozi wa chama chao kwa kuitisha mkutano wa wanachama pamoja na kufanya uchaguzi.
“Ofisi ya bodi ya filamu kwa kushirikiana na wadau wa warsha hii imeadhimia kuandaa mafunzo ya siku tano kwa waandajia na wapiga picha wa kazi za filamu wa halmashauri ya Tunduma ili kuwa jengea uwezo mzuri kutoka na maombi waliyoya wakilisha,”alisema Bi. Fissoo.
[caption id="attachment_33819" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw.Juma Mhina alimhakikishia Mheshimiwa naibu waziri huyo kupokea ombi na kuliwakilisha la wadau hao wa sekta ya filamu kuomba kupatiwa msaada wa kisheria katika uandaaji wa mikataba kutoka kwa wataalamu wa sheria waliyoko katika ofisi za mkoa na halmashuri .
Pamoja na hayo nae mmoja wa waigizaji kutoka halmashauri ya mbozi Bi. Magreth Seme aliyeshiriki warsha hiyo aliishukuru bodi ya filamu nchini kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa mafnzo hayo kwani yapo mengi waliyojifunza ambayo yatasaidia kuboresha kazi zao za filamu.