Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shirika la Posta Tanzania Lapata Gawio la Fedha kutoka Benki ya Posta
Jul 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_5577" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akipokea gawio la hisa ya Shirika hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Benki ya Posta Tanzania, Prof. Leticia Mutayobya.

[/caption] [caption id="attachment_5576" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea gawio la hisa la shilingi bilioni 1.032 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, Prof. Leticia Mutayobya.[/caption] [caption id="attachment_5578" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akimueleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango ambapo aliiomba Serikali kupitia kuilipa Shirika la Posta Tanzania shilingi bilioni 3.6[/caption]

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango  leo amepokea hundi ya shilingi bilioni 1.032 kutoka kwa Benki ya Posta Tanzania ikiwa ni gawio la hisa ya asilimia 86.17 kwa Serikali kama mmoja wa wanahisa kwenye Benki hiyo.

Akikabidhi hundi hiyo mjini Dodoma Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Prof.Leticia Mutayoba, amesema makabidhiano hayo ni katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kukusanya mapato yake yenyewe kutoka kwenye vyanzo vyake na kuepuka utegemezi kutoka kwa wahisani.

Pia Prof.Mutayoba alimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania Dkt. Haruni Ramadhan Kondo hundi ya shilingi milioni 97.8 ikiwa ni gawio la hisa ya asilimia 7.98 kama mmoja wa wanahisa wa Benki hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango amezitaka Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kuilipa Serikali gawio la hisa zake na zijiendeshe kwa ufanisi na kwa faida ili makusanyo hayo yaweze kuwahudumia wananchi.

Katika tukio hilo, Dkt. Kondo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iweze kuilipa Shirika la Posta Tanzania shilingi bilioni 3.6 ambazo ni malipo ya pensheni ya wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Shirika limelipa pensheni hizo kwa niaba ya Serikali.

Utaratibu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kulipa gawio la hisa kwa Serikali na wanahisa wengine ni maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma yanafanya kazi kwa ufanisi, kuzalisha faida na kutoa gawio kwa Serikali ili mapato hayo yaweze kuhudumia wananchi katika Nyanja mbali mbali kama vile huduma za afya, elimu, maji na barabara.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Dkt. Maria Sasabo, Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Deogratius Kwiyukwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi