Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yazungumzia Mauaji Kibiti
Jun 30, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4870" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na. Eliphace Marwa

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni  Hamad Masauni amekutana na vingozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika kikao cha kujadili hali ya ulinzi na usalama nchini  mara baada ya kufanya ziara hapo jana katika Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kikao hicho Naibu Waziri Masauni Hamad Masauni amewataka wananchi kuwa na amani kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu nchini.

[caption id="attachment_4873" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha baadhi ya picha za watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Si muda mrefu hali ya usalama rufiji itakuwa nzuri kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na kazi na matatizo yote yatapatiwa ufumbuzi muda si muda mrefu,” alisema Naibu Waziri Masauni.

Aidha Naibu Waziri Masauni amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kusema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwadhibiti wahalifu wawili kabla hawajatekeleza uhalifu.

Naibu Waziri Masauni amevitaka vyombo vya habari kuwatoa hofu wananchi kwani mpaka sasa wamepata picha 16 za washukiwa wa mauaji ya Kibiti na Rufiji na kusema mpaka sasa kazi inakwenda vizuri.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema kuwa kuna changamoto ya miundombinu katika maeneo ambayo washukiwa hujificha kuwa si rafiki kutokana na umbali na kutokuwa na njia za magari kupita hivyo jeshi la polisi limepanga kuanzisha doria ya pikipiki katika maeneo yote yanayohisiwa kuwepo na wahalifu.

 “Wananchi wanatoa taarifa sasa niseme kwa lugha nyingine wanafunguka kama mmepata taarifa majambazi wanne wameuwawa na silaha mbili za kivita zimepatikana mimi  niwapongeze sanasana waliotupa zile taarifa na waendelee hivyohivyo naamini kwa mwendo huo tutafika salama,”alisema IGP Sirro.

Alimtaja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Onesmo Lyanga  kuwa atakaimu kama Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Rufiji kwani lengo kubwa ni kunafikisha huduma karibu na wananchi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi