Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali yawajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya Ukimwi
Nov 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi wa masuala ya Ukimwi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya wakati wa warsha ya wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14, 2017.[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Utafiti na Tathimini Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akiwasilisha mada ya hali ya UKIMWI nchini kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika tarehe 14 Novemba, 2017.[/caption]

Na.MWANDISHI WETU

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Taifa yakudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imedhamiria kuendelea kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi ili iweze kushiriki vyema katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

Akizungumza wakati wa Semina ya siku tatu iliyoanza leo mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi inafanikiwa ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Dr. Leonard Maboko akichangia hoja kuhusu masuala ya Ukimwi wakati wa Warsha ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya iliyofanyika Mjini Dodoma.[/caption]

“Serikali imejipanga kuhakikisha swala hili linapewa kipaumbele hasa katika kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI” Alisisistiza Mhe. Mhagama

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi niya kila Mtanzania hivyo ni vyema wadau wote wakashirikiana na Serikali katika mapambano hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi Mhe. Daniel Mtuka amesema  Warsha hiyo inajenga msingi kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake.

Aliongeza kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na Ukimwi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa  malengo yakuondoa janga hilo hapa nchini yanatimizwa kwa wakati muafaka.

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe.Zainab Bullu akifafanua jambo wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi.[/caption]

Kwa Upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Mhe. Martha Mlata amesema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Janga la Ukimwi kwa kusimamia maadili katika Jamii hali itakayochochea kuleta mabadiliko.

Warsha ya Siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi inafanyika mjini Dodoma kwa siku tatu ikilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi