Na Mathias Canal, WEST – Dodoma
Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini.
Katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni Mia moja (100 Bil).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema hayo leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Jimbo Manyoni Mashariki aliyetaka kufahamu Serikali ina Mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Manyoni.
Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi.
Aidha, Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.
Waziri Mkenda amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2022/23, Serikali imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi.
Aidha, Prof. Mkenda amesema kuwa Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.
Waziri Mkenda amewashauri wananchi wa Wilaya ya Manyoni wakiwemo wa Jimbo la Manyoni Mashariki waendelee kutumia Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Singida na Chuo cha Wilaya ya Ikungi pamoja na Vyuo vya Singida na Msingi FDC na Vyuo vingine vya ufundi stadi vilivyopo nchini.