Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yashirikiana na Kampuni ya Simu Kusaidia Watoto na Wanawake
Jun 30, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_44800" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Joseph Kandege akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Jamii kutoka vodacom ( Social Impact Report and new strategy to deliver inclusive growth) inayohusu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, uliofanyika Juni 27, 2019, Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Lailat Abeid MAELEZO

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya Afya, Elimu  na Miundombinu.

Akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Naibu  Waziri wa  Tamisemi,  Joseph Kandege amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia watanzania wote wenye mahitaji .

 Waziri kandege Amesema Vodacom wanafanya   kazi ambazo zinagusa jamii kama afya   na kuwasaidia watoto wa kike kwenda shule kwa kuwapatia vitaulo vya kujihifadhia katika hedhi, pia wameendelea kuwasaidia kina mama juu ya ugonjwa wa fistula ambayo inawapelekea wamama wengi kutengwa na jamii.

“ Serikali itahakikisha inaimarisha miundombinu ili kuhakikisha vodacom inawafikia  watu wenye uhitaji na pia tumeona jinsi walivyoweza kuwasaidia watoto wa kike na wakinamama wenye fistula juu ya kupata matibabu  ya ugonjwa huo na kugawa vitaulo kwa watoto wa kike wenye uhitaji, ambao wanakosa kwenda shuleni pindi wawapo kwenye hedhi”.

[caption id="attachment_44801" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Joseph Kandege, akikata utepe kuzindua Ripoti ya Jamii kutoka Vodacom ( Social Impact Report and new strategy to deliver inclusive growth) inayohusu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, uliofanyika Juni 27, 2019, Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Kilimbe, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania na Afisa Mahusiano wa Taasisi hiyo, Rosalynn Mworia na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Hashim Hendi.[/caption]

Amesema matarajio yake ni kuwa  kazi inayofanywa na vodacom  iweze kufanywa na mashirika mengine kwa kushiriki jambo kama hilo au kwa kujiunga pamoja na vodacom kufanya jambo hilo.

“ Matarajio yangu kazi hii inayofanywa na Vodacom isiwe yao na  hayo mashirika wanayoshirikiana nayo, kwani hili ni jambo la kitaifa, hivyo ni vyema mashirika mengine hata ya watu binafsi wakaendeleza juu ya hili, au wakaanzisha mambo kama haya ilikuweza kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ujumla” .

Aidha  Mkuurugenzi wa  Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation  na Afisa Uhusiano,   Rosalynn Mwaria  amesema wamekuja kuonyesha matokeo chanya ya kazi walizokuwa wakizifanya kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, wakiambatana na sekta binafsi pamoja serikali kwa kuwasaidia watoto na kinamama kwenye mambo mbalimbali .

Amesema hadi kufikia hapa wameshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimewawezesha kufikia wanawake  kwa upande mkubwa  na kwa watoto wa kike kwenye sekta ya  Elimu , Afya na pia kuwawezesha kiuchumi katika mambo tofauti ili kuiendeleza Tanzania na  kuifikia jamii.

[caption id="attachment_44799" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo, Rosalynn Mworia akizungumza kuhusu uzinduzi wa Ripoti ya Jamii kutoka Vodacom (Social Impact Report and new strategy to deliver inclusive growth) inayohusu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, uliofanyika Juni 27, 2019, Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa mwaka 2019 hadi 2021, Mkurugenzi huyo amesema wamejikita  katika miradi ya  watoto katika  Elimu  na pia kufanya maendeleo ambayo yatawasaidia kutunza mazingira ya Tanzania nzima.

“ Hadi kufikia hapa tumeshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimetuwezesha kuwafikia watoto wa kike na wanawake katika kuwasaidia kwenye Afya pamoja na kiuchumi kwa mwaka 2019 hadi 2021, tumejikita katika kuwasaidia watoto wa kike pia kufanya maendeleo ambayo yatatusaidia kutunza Mazingira ya Tanzania “.

Pia amesema watajikita zaidi katika maeneo ya Elimu na kiuchumi kwa ujumla ili kuweza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati ilikuweza kujikwamua kutoka pale walipo ilikuweza kusaidia Taifa kufikia uchumi wa kati kwa mwaka 2025.

“Tutajikita katika maeneo ya Elimu na Uchumi kwa ujumla ili kuweza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati kwa ujumla kujikwamua kutoka pale walipo ilikuweza kusaidia Taifa kufikia Uchumi wa kati mwaka 2025”.

[caption id="attachment_44798" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Joseph Kandege (katikati) akifurahia jambo na Kamishna wa Polisi (mstaafu) Suleiman Kova wakati akiwasili kuzindua Ripoti ya Jamii kutoka kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ( Social Impact Report and New Strategy to Deliver Inclusive Growth) inayohusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo, uliofanyika Juni 27, 2019, Jijini Dar es Salaam. Nyuma ya Kamishna Kova ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia.
                                                                     (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)


[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi