Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yapunguza Idadi ya Hati Chafu
Apr 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30216" align="aligncenter" width="888"] Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2017.[/caption] [caption id="attachment_30219" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad leo mjini Dodoma kuhusu ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2017.[/caption]

Na Mwandishi Wetu.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea vizuri na uwekaji wa mahesabu uliopelekea kupungua kwa hati chafu katika Taasisi na miradi mbalimbali ya Serikali.

Prof. Assad  ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017.

[caption id="attachment_30218" align="aligncenter" width="788"] Mbunge wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya LAAC mara baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2017.Katikati ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC mhe. Naghenjwa Kaboyoka.[/caption]

"Katika ukaguzi wa hesabu nilioufanya katika Serikali Kuu na Taasisi zake, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2016/17 nimetoa jumla ya Hati 561 za ukaguzi. Kati ya hati hizo, Hati zinazoridhisha ni 502 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 8, Hati zisizoridhisha ni Saba sawa  na asilimia Moja na Hati Mbaya ni Saba sawa na asilimia Moja," alisema Prof. Assad.

Amesema, katika ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ametoa jumla ya Hati za Ukaguzi 742 ambapo Hati zinazoridhisha ni 697 sawa na asilimia 94, Hati zenye shaka ni 44 sawa na asilimia 5.9 na Hati isiyoridhisha ni moja, Hati hii imetolewa kwa mradi wa maji (WSDP) unaotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Wilaya ya Makete.

[caption id="attachment_30217" align="aligncenter" width="900"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali baada ya CAG kuwasilisha ripoti za Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2017.[/caption]

Naye, Mjumbe wa Kamati ya LAAC Mhe. Abdallah Mtolea amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kuonekana kupunguza idadi ya hati chafu na kushamiri kwa hati safi.

Aidha Mhe. Mtolea amesema kuwa kamati hiyo itaziita Halmaushari na kufanya nazo mahojiano bila kuujali matokeo ya ukaguzi kama zilifanya vizuri au vibaya ili kuhakikisha kuna kuwa matumizi mazuri ya fedha za umma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi