Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yapongezwa kwa Kuwainua Wanawake Sekta ya Madini
Jul 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33541" align="aligncenter" width="900"] Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Madini, Kampuni ya InterConsult Ltd, SUMA JKT na Chuo cha Madini wakitoka eneo litakapojengwa jengo la gorofa 3 katika chuo cha madini mjini Dodoma litakalotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaoshiriki katika uchimbaji wa madini.[/caption]

Frank Mvungi- Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa kuweka kipaumbele katika kuwainua Wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini hapa nchini.

Akizungumza katika  mahojiano maalum mjini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi eneo litakapojengwa jengo la ghorofa 3 katika Chuo cha Madini likilenga kuwainua Wanawake wote wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini kupitia Chama cha Wachimbaji Wanawake, Makamu mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Chuo hicho Bw. Fedrick Mangasini amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo Serikali imedhamiria kuwainua wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini.

 “Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchimbaji wa madini kwa kuzingatia weledi na sheria zilizopo,” alisisitiza

[caption id="attachment_33542" align="aligncenter" width="863"] Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akionesha mipaka ya eneo kitakapojengwa kituo maalum kitakachotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association),jengo hilo lenye gorofa tatu linajengwa katika chuo cha madini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33543" align="aligncenter" width="827"] Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akimkabidhi Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi David Palangyo ramani ya jengo la ghorofa tatu linalojengwa na SUMA JKT katika chuo cha madini Dodoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Endelevu wa Rasilimali Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project- SMMRP), mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha sekta hiyo na kukuza uchumi.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa Kituo hicho kitanufaisha wanafunzi wa chuo hicho na wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini kwa kuwa itakuwa fursa kwao kujengewa uwezo wa kushiriki kikamilifu katika kukuza sekta hiyo na kuwainua kiuchumi.

Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project- SMMRP) ukilenga kuboresha sekta ya  madini nchini hususan kwa wachimbaji wadogo ili kuwaongezea ujuzi katika eneo la uchimbaji madini na kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi ……. Amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa wanakamilisha mradi huo kwa wakati mara baada ya kukabidhiwa eneo la ujenzi na ramani za jengo hilo linalojengwa chuo cha madini Dodoma.

Ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la chuo cha Madini Dodoma utagharimu zaidi ya Bilioni 11 ambapo mradi huo ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha sekta ya madini hapa nchini na kuchochea ustawi wa wachimbaji wadogo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi