Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yajipanga Kukuza Lugha ya Kiswahili
Jun 28, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

[caption id="attachment_4654" align="aligncenter" width="752"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Idhaa hiyo hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Profesa Riyah Timamy. Maadhimisho hayo yalifanyika jana Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Zawadi Msalla

Serikali imeahidi kuweka misingi madhubuti ya kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuhakikisha lugha hiyo inatumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo kufundishia katika taasisi za kielimu, Mahakamani na Bunge.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)jana Jijini Dar es Salaam.

[caption id="attachment_4655" align="aligncenter" width="752"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisikiliza mdahalo mbashara kupitia kipindi cha Dira ya Dunia kuhusu lugha ya Kiswahili wakati wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uoingereza (BBC). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Profesa Riyah Timamy na wanaofuata kulia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Chambogo cha Kampala Uganda, Dkt. Ida Mtengo na Mhariri Mwandamizi kutoka BAKITA, Oni Sigala. Maadhimisho hayo yalifanyika jana Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa Wizara yake ipo katika hatua za ukamilishaji wa kuundwa kwa sera mpya ya Lugha ambayo itasimamia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili na kufanya matumizi ya lugha hiyo kukuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Serikali imejipanga kukifanya kiswahili kuwa kati ya lugha tatu bora duniani, kwa sasa ni miongoni mwa Lugha 10 maarufu kati ya lugha 6000 na ya pili kutumika barani Afrika” alieleza Waziri Mwakyembe.

[caption id="attachment_4656" align="aligncenter" width="752"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea keki kutoka kwa Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Bi. Liz Masinga wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Idhaa hiyo hapa nchini. Kulia ni Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Oni Sigala. Maadhimisho hayo yalifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalifanyika jana Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Aliongeza kwa kueleza kuwa uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa lugha hiyo adhimu huku Serikali ikihakikisha Kamusi hiyo inasambazwa katika maeneo yote muhimu zikiwemo ofisi zote za Balozi za Tanzania nje ya nchi, Taasisi za Elimu kuanzia ngazi za awali hadi za juu na mahakamani.

Vilevile Mhe. Mwakyembe amewapongeza wafanyakazi na uongozi wa Idhaa ya Kiswahili BBC kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inatumika katika matangazo yao na kukifanya kusikiwa dunia kote.

Aidha Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania wote kukipenda na kukienzi Kiswahili kwani ndiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kila mtanzania mahali popote pale duniani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi