[caption id="attachment_37790" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/2020 bungeni leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37791" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikabe Waitara (CCM), akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakati wa kikao cha kwanza Bunge la 13 leo jijini Dodoma. Wabunge wanne wameapishwa baada ya kuchagulia kutokana na kuhama vyama vyao. Wabunge hao ni Julias Kallanga (Monduli – CCM), Mhe. Kuchauka (Liwale – CCM), pamoja na Thimotheo Mnsava ( Korogwe Vijijini –CCM) aliyechukua nafasi ya Stevene Ngonyani (Majimarefu aliyetangulia mbele za haki).[/caption] [caption id="attachment_37792" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimskiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maenddeleo ya Makzi, William Lukuvi (kushoto) wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37793" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wakifuatilia kitabu cha Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2019/2020 katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37794" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangallah (kushoto) wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Janeth Massaburi.[/caption] [caption id="attachment_37795" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37796" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo wakati wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kandege.[/caption] [caption id="attachment_37797" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akijibu swali wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37798" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wageni wakifuatilia kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.[/caption]