Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaipa RAHCO Wiki Mbili Kusafisha Maeneo Yote Waliyoyabomoa Dodoma Mjini.
Feb 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28682" align="aligncenter" width="750"] Muwakilishi wa RAHCO Bw. Athuman Muya akimuongoza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola kukagua hali ya uchafuzi wa Mazingira eneo la Stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Dodoma mapema leo, eneo hilo linamilikiwa na RAHCO.[/caption]

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetoa muda wa wiki mbili kwa Kampuni Hodhi ya Rasimali za Reli (RAHCO) kusafisha maeneo yote yaliyobomolewa na kampuni hiyo ikiwemo stendi kuu ya mabasi Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola ametoa agizo hilo leo mkoani Dodoma alipotembelea na kukagua eneo la stendi hiyo ambalo lilibomolewa na RAHCO kwa ajili ya kupisha ujenzi wa reli ya kisasa.

[caption id="attachment_28683" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola (mwenye traksuti) akikagua eneo la stendi ya mabasi Mkoani Dodoma ili kujionea hali utunzaji wa Mazingira katika eneo hilo ambapo alitoa maelekezo kwa Kampuni Hodhi ya Rasimali za Reli (RAHCO) kama mmiliki wa eneo hilo kuhakikisha kuwa mazingira ya eneo hilo yanakuwa safi kufuatia uboaji wa Vibanda uliofanyika katika eneo hilo hivi karibuni hali iliyosababisha uchafuzi wa mazingira.[/caption] [caption id="attachment_28684" align="aligncenter" width="859"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola (mwenye traksuti) akionesha uchafuzi wa mazingira uliofanywa katika eneo la stendi ya Mkoa wa Dodoma wakati akikagua hali ya mazingira katika eneo hilo mara baada yakubomolewa kwa Vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo katika eneo hilo linalomlikiwa na RAHCO.[/caption]

“Kulikuwa na zoezi la ubomoaji katika eneo hili la stendi lakini baada ya uboaji hakuna usafi wowote uliofanyika na kampuni ya RAHCO ambayo ndio iliyofanya zoezi hilo la ubomoaji,” alisema Lugola.

Aliendelea kwa kusema eneo hilo limeachwa likiwa na mabaki ya mbao, matofali, misumari, na mabati yakiwa yameenea kila eneo hivyo kulifanya eneo hilo la stendi kuwa chafu.

Hivyo basi Mhe. Lugolai amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO kuhakikisha analisafisha eneo hilo na kulizungushia uzio ili kuzui kuendelea kuchafuliwa kutokana na eneo hilo kuwa wazi.

[caption id="attachment_28685" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola akiwaonesha waandishi wa habari na wananchi hali yauchafuzi wa mazingira katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Mkoani Dodoma ambapo aliiagiza RAHCO kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika ene hilo kwa kuwa Dodoma sasa ni Makao Makuu ya Nchi.[/caption] [caption id="attachment_28686" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola akiendelea kukagua eneo hilo la Stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Dodoma mapema leo.[/caption]

[caption id="attachment_28688" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola akiwa na wananchi wanaofanya biashara ndogo ndogo katika eneo la Stendi Kuu ya mabasi Mkoani Dodoma wakati wa ziara yake katika eneo hilo.(Picha zote na Frank Mvungi – MAELEZO, Dodoma)[/caption]

Lugola amesema Mji wa Dodoma kupitia Manispaa yake una maeneo ambayo yametenga kwa ajili ya stendi, hivyo stendi itahamishiwa eneo hilo lililotengwa mara tu baada ya kukamilika.

Aidha mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Ndugu Zakaria Mmari aliuliza juu ya kufikiriwa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo kuendelea kufanya biashara mpaka pale stendi mpya itakapokamilika.

“Yote mliyoyaeleza nimeyachukua na nitaenda kufanyia kazi na mtajulishwa majibu ya ombi lenu,” alijibu Lugola.

Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia idara ya Mazingira imeanzisha programu maalum ya kuifanya Makao Makuu ya Nchi kuwa ya kisasa ikiwa ni pamoja na kuikijanisha kwa kupanda miti katika maeneo yote ya mkoa huo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi