Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yagawa Vitendea Kazi kwa Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI
Aug 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_34510" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama funguo za magari waliyoyatoa kwa ajili ya Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI, hivi karibuni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.[/caption] [caption id="attachment_34512" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akionesha funguo za magari waliyokabidhiwa na Marekani kwa ajili ya Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma, katikati ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndema.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Serikali imeongeza nguvu za uratibu wa udhibiti UKIMWI nchini kwa kutoa vitendea kazi kwa Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI nchini katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Vitendea kazi vilivyotolewa ni pamoja na magari 5 na vifaa bongine vya ofisi zikwemo komputa katika Mikoa ya Mbeya,Katavi,Rukwa,Ruvuma na Songwe.

Lengo la kuwezesha Mikoa hiyo ni kuhakikisha uratibu wa UKIMWI nchini unaratibiwa ipasavyo kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa,Kata,Halmashauri,Mkoa hadi Taifa. Awali Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS) Dr Leonard Maboko akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Serikali ni kudhibiti maambukizi mapya ya VVU na hii itawezekana endapo uratibu utaimarishwa kuanzia ngazi ya jamii.

Dr Maboko aliongeza kuwa anaamini kuwa baada ya kukabodhowa vitendea kazi hivi, Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI wa TACAIDS katika Mikoa watakuwa hawana kipingamizi katika utendaji wa kazi na kuwafikia wananchi ,ikiwa ni pamoja na kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa wakati.

[caption id="attachment_34509" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akiwasha Moja ya Gari waliyokabidhiwa na Ubalozi wa Marekani hivi Karibuni, Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.[/caption]

Dr Maboko amewaasa Waratibu hao kuakikisha wanatunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa manufaa ya Serikali na sio manufaa binafsi.

Naye waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama alisema kuwa hali ya maambukizi ya vvu nchini inatutahadharisha kuwa ni lazima kuwa na mbinu mbadala za kukabiliana na maambukizi mapya.

Kwa sababu hiyo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Idara yake ya Ulinzi (DOD)ilianzisha Mkakati wa Kikanda wenye kulenga mazingira na vichocheo vinavyofanana katika Mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma ili kukabiliana na maambukizi ya VVU kwa kuunganisha nguvu na rasilimali.

Mhe Mhagama aliongeza kuwa hadi sasa kila Mkoa tayari umetengeneza Mpango Mkakati wa Mkoa wa Kudhibiti UKIMWI kulingana na vihatarishi vilivyotajwa kwenye utafiti wa viasharia vya VVU na UKIMWI vya mwaka 2016/2017 aliagiza viongozi wote kushiriki katika kutekeleza Mwitikio wa UKIMWI kwa kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika mpango mkakati ulioainishwa na Mkoa husika katika maeneo ya kinga ,matunzo na matibabu ili kupunguza athari zitokanazo na UKIMWI.

[caption id="attachment_34514" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akionesha funguo baada ya kupokea magari kutoka Waziri Jenista Mhagama (kulia) aliyekabidhiwa na Ubalozi wa Marekani,[/caption]

Naye kaimu Balozi wa Marekeni alisema kuwa lengo la ushirikiano wa Marekeni ni kuwawezesha watanzania kufanya kazi ya kujenga nchi imara ,yenye afya na ustawi zaidi,"nami ninafurahi kuendeleza mtizamo huu kuhakikisha kwamba jamii ya Watanzania waliojitoa na kuwa na dhamira ya dhati,wanapata nyenzo zinazohitajika katika kujenga maisha bora ya baadae" Aidha Serikali ya Marekani inajivunia kuunga mkono jitihada nyingi za ushirikiano kwenye masuala ya Afya,ikishirikiana na Watanzania ili kuimarisha uwezo wa kushughulikia malaria,Afya ya mama na mtoto,uzazi wa mpango,Kifua kikuu,Lishe, VVU na UKIMWI.

[caption id="attachment_34515" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko (wa kwanza kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia)[/caption]

Aliongeza kuwa magari sita yaliyonunuliwa yatasaidia kuboresha uratibu na uwajibikaji kwenye programu za UKIMWI za Mikoa kuboresha usimamizi na uangalizi katika Mikoa na Makao Makuu ya TACAIDS katika kuboresha afya katika Nyanda zaJuu Kusini.

[caption id="attachment_34517" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko( kulia) akimkabidhi funguo za gari Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Ruvuma Bw. Daniel Mwaiteleke Baada ya kupokea magari hayo kutoka Ubalozi wa Marekani, anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama.[/caption]

Magari sita yaliyokabidhiwa kwa TACAIDS yameenda katika Mikoa mitano ya Mbeya,Rukwa,Katavi,Songwe na Ruvuma na moja limebaki TACAIDS kwa ajili ya usimamizi wa program.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe Christine Mndeme alishukuru kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini kupatiwa msaada huo kwa kuwa mikoa hiyo ndio yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU na UKIMWI,kwa kubuniwa mradi huo kutasaidia zaidi katika kuongeza ushirikishwaji wa jamii katika kupambana na maambukizi ya VVU.

Kwa kufanya hivyo wanjamii wataelewa kuwa wanao wajibu mkubwa wa kufanya ili kukabiliana na maambukizi ya VVU badala ya kutegemea serikali na wadau wa maendeleo pekee.

Mhe Mndeme aliongeza kuwa mradi huu umekusudia kushirikisha viongozi wakuuwa siasa kama wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kusimamia Mwitikio wa UKIMWI ili kuongeza uwajibikaji

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi